TITO KASAMBALA ALIPOKAMATA CPA YAKE MHASIBU HOUSE!!

Tito Kasambala akipozi kwa picha na maiwaifu wake Vicky baada ya kupokea CPA yake kwenye mahafali ya NBAA yaliyofanyika jumamosi iliyopita kwenye viwanja vya Mhasibu House jijini Dar es salaam na kufuatiwa na sherehe ya kukata na shoka kwenye mgahawa wa City Garden.
Mdau Tito na Mke wake katikati wakiserebuka na mama yao kushoto wakati wa sherehe hiyo ya kujipongeza baada ya kukamata CPA yake pale Mhasibu House jumamosi iliyopita.
Tito na Mke wake Vicky wakijiandaa kumlisha keki dada ya Flora Kasambala ambaye alielezewa na Tito mwenyewe kuwa ni mtu muhimu sana kwa mafanikio yake.
Salome na Oliver wakipoozi kwa picha.
Dada Tina Malasusa kushoto na rafiki yake nao walikuwepo kumpa tafu Tito.
Mdau Tito Kasambala akiwa katika picha ya pamoja na ndugu na jamaa mara baada ya sherehe yake ya kujipongeza kwa Nondooz zake za CPA iliyofanyika katika mgahawa wa City Garden jijini Dar mwishoni mwa wiki.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. yaani ilikuwa ni full shangwe!!
    siyo mchezo kaka nakufagiliaaaaaaaaaaaaaaaa sana brother!! yaani nikikumbuka jinsi ulivyoanza kwa taabu lkn mungu ni mweza wa yote amekufanikisha !! ubarikiwe sana kaka!! Thanks my wifi kwani umeonyesha support nzuri sana hadi mzee kafanikisha CPA yake!! Dada flora umeng'aaa kama jina lako dada!! aah mama Kasambala umetoka bomba sana!!

    Mzee Boss nakuona kaka unang'aa sana hiyo suti yako balaa!!!!
    dada Tina na mwenzio yaani hizo za Africana kabisa mambo ya Africa magharibi!!

    Otherwise wote naona mpo safi sana yaani mmependeza!!

    Mungu akubariki sana kaka Tito ila usinisahau ktk ufalme wako maana CPA hii najua mungu ameisha bariki italeta Range rover(Vogue) hiyo brother!! be blessed!! your sisy Alice

Post a Comment