SELESTIN MASSANJA MENEJA WA UWANJA WA TAIFA AFARIKI DUNIA!!

Marehemu Selestin Massanja aliyeko katikati katika picha enzi za uhai wake akiwa katika moja ya shughuli zake za michezo kama meneja wa uwanja wa Taifa.
Kaimu katibu mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Bw. Gasper Mwombezi akizungumza na wandishi wa habari asubuhi hii kwenye ukumbi wa Idara ya Habari maelezo alipotangaza kifo cha Ghafla cha Meneja wa viwanja vya Uhuru na uwanja mpya waTaifa kilichotokea usiku wa kuamkia leo baada ya kuangukiwa na ukuta na kukimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili ambako baadae alifariki dunia Bw. Gasper amesema habari zaidi zitatolewa baadae lakini Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo imeunda kamati ili kushughulikia masuala yote kuhusiana na msiba huo katika picha kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Clement Mshana.
Selestin Masanja alizaliwa Urambo Mkoani Tabora Januari 20 mwaka 1957 na kusoma elimu ya msingi na hapo baadae alijiunga na shule ya Sekonsari ya Itagana 1972-1975 baadae shule ya Sekondari Minaki 1975-1977.
Mwaka 1988 alienda nchini Cuba katika jiji la Havana na kuchukua shahada ya Uzamili wa Physical Education.
Akiwa mfanyakazi wa Serikali katika idara ya Michezo Marehemu Massanja aliwahi kuwa Afisa michezo mkuu daraja la I, Meneja wa uwanja wa Taifa, Mjumbe wa kamati ya Ufundi ya TFF, Katibu mkuu wa FAT Msaidizi, Afisa michezo idara ya Michezo, Katibu mkuu msaidizi wa FAT tena na akawa Kocha Mkuu wa African Sport ya Tanga

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment