MASHINDANO YA SHIMIWI YARINDIMA MKOANI MOROGORO!!

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mwantumu Mahiza akihojiwa na Mwandishi wa habari kutoka TBC1 Jeni John mara baada ya timu yake ya Netball kuibuka na ushindi katika mashindano ya SHIMIWI
Mchezaji wa timu ya Ofisi ya waziri mkuu William Benjamin (kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Wizara ya elimu Gunda Azizi wakati wa ufunguzi wa michezo ya SHIMIWI iliyozinduliwa mjini Morogoro mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na kampun i ya simu zamkononi ya Vodacom ambapo Wizara ya Elimu iliibuka kidedea kwa kushinda magoli 2-0 dhidi ya timu ya Waziri Mkuu.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya kilimo wakivuta kamba wakati wa mashindano ya SHIMIWI yaliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Morogoro na kudhaminiwa na Kampuni ya Vodacom kilimo iliiwashinda timu ya Moa wa Lindi kwa kuwashinda kuvuta kamaba mara mbili.(Picha na Rajabu Mhamila)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment