IBUA FILM STAR WAMWAGA SERA YA KUIBUA VIPAJI VYA WAIGIZAJI NCHINI!!

Mkurugenzi wa masoko wa YEC Production Bw. Adam Sesilo akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo juu ya shindano la kuibua vipaji vya uigizaji kwa wasanii chipukizi nchini.
Sesilo amesema mchakato rasmi wa kutafuta vipaji hivyo unaanzia katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Mbeya, Zanzibar, Mwanza na Dar es salaam, ameongeza kuwa vigezo vya washiriki vitakuwa ni miaka 16 na kuendelea lakini pia washiriki wawe na akili timamu, wawe pia wanaweza kusoma na kuandika
Mshindi wa IBUA Film Star Tanzania atajinyakulia zawadi nono ambayo itatangazwa hapo baadae, fomu za kushiriki kwenye shindano hilo zinapatikana mikoa husika ambayo ni Arusha Club Silk, Mwanza Salma Cone, Mbeya CPMTL Stationary mkabala na ofisi ya mkuu wa mkoa, Dodom Zunny Ice cream Parlour,Zanzibar ofisi za Zenj FM, Dar es salaam TCC Chang'ombe, Shear Illusions Mlimani City Royal Saloon Sinza, Zizzou Fashion Sinza na fomu hizo zitaanza kupatikana oktoba 10 mpaka novemba 1
Katika shindano hilo watatafutwa washiriki 50 na kuwekwa kambini ambapo watachujwa na majaji na kubakia washinriki 20 ambao watatengeneza filamu kwa pamoja na waigizaji wazoefu kutoka YEC Productuions wengine wanaofuatia katika picha ni Adam Selemani Swebe meneja Uzalishaji, Jaquline Wolper balozi wa IBUA FILM STAR na Jennifer Mwaipaja Balozi wa IBUA FILM STAR.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment