SIMBA YAITAFUNA TOTOAFRICA KWA BIBI, YANGA WANYWA CHUPA MOJA YA MAJI SONGEA!!


Ligi kuu ya Vodacom imeendelea kurindima katika viwanja tofauti nchini ambapo katika uwanja wa uhuru maarufu kama shamba la bibi Simba Sports Club iliwakaribisha Toto Africa kutoka mwanza katika mchezo huo uliokuwa mkali simba imeivurumisha timu hiyo kutoka kanda ya ziwa magoli 3-1 yakifungwa na wachezaji Mussa Hassan Mgosi kwa penati iliyopatikana katika dakika ya 45 kabla ya timu hizo kwenda mapumziko,
Baada ya timu hizo kurudi katika kipindi cha pili simba iliweza kutumia nafasi ilizopata vyema ambapo iliweza kupata magoli mengine mawili kutoka kwa wachezaji wake Haruna Moshi (Boban) na mchezaji Okwi hivyo kuifanya simba kushinda magoli 3-1 na kujikusanyia jumla ya pointi 9 goli pekee la Toto Africa lilifungwa na mchezaji Rawlence Mugia.
Katika uwanja wa Majimaji huko Somgea Majimaji imeweza kuinywesha chupa moja ya maji timu ya Yanga goli ambalo lilifungwa na mchezaji Thomas Morris katika dakika ya 60 ya mchezo huo goli hilo lilitosha kabisa kuikosesha Yanga pointi tatu timu hiyo ya Dar es salaam kutoka mtaa wa jangwani, hivyo kuifanya ilale bao 1-0 mbele ya wanalizombe hao ambao wamepokea vichapo viwili mfurulizo kutoka kwa simba na JKT Ruvu ya Pwani katika michezo yake iliyopita,

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment