Mtangazaji wa TBC1 Enock Bwigane akiwa amepozi na mke wake Miriam Lumelezi nje lango kuu la kanisa KKKT Azania Front mara baada ya kufunga ndoa yao kanisani hapo mchana leo, Mke wake ni Mfanyabiashara na sherehe yao itafanyika kuanzia jioni kwenye ukumbi wa Helenic Posta Jijini Dar es salaam FULLSHANGWE inawapa shavu maharusi hao na inawatakia maisha mema na yenye furaha na mafanikio katika ndoa yao.
Enock Bwigane na Mkewe Miriam Lumelezi pamoja na wapambe wao wakipozi kwa picha pamoja na mchungaji kwa nyuso za furaha, mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu katika kanisa la KKKT Azania Front mchana huu.
Ndugu na jamaa wa Mtangazaji wa TBC1 Enock Bwigane wakicheza na kufurahi mara baada ya mtangazaji huyo kufunga pingu za maisha na mkewe Miriam Lumelezi mchana huu kwenye kanisa kuu la KKKT Azania Front Mkewe ni mfanyabiashara na nda hiyo itafuatiwa na sherehe ya kukata na mundu pale kwenye ukumbi wa Helenic Posta jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment