Mkazi wa Mbagala kuu Aisha Amanzi akielezea waandishi wa habari jinsi hali ilivyokuwa mara baada ya mlipuko huo uliotokea leo asubuhi huko Mbagala kuu karibu na kambi ya Jeshi la wananchi na kuuwa watoto wawili Rajabu Said miaka 5 na Regina Christian Chavala wakati wakipokuwa wakicheza katika eneo ambalo takataka zilikusanywa na kuchomwa moto ili kufanya usafi kitu kilichofanya mabaki ya mabomu yaliyolipuka hivi karibuni katika kambi hiyo kulipuka,
Watoto waliojeruhiwa katika tukio hilo ni Saada Selemani, Asha Selemani na Stella Christian Chavala ambaye amejeruhiwa vuibaya na kukimbizwa hospitali ya Muhimbili kwa Matibabu zaidi
Mkazi wa Mbagala kuu mama Eva Paulo katikati akiwa na watoto wake Asha Suleiman miaka 5 Kulia na Saada Suleiman miaka 2 walionusurika katika ajali ya bomu hilo wakipata kifungua kinywa mara baada ya kupata matibabu hospitalini na kuruhusiwa kurejea nyumbani familia hii pia imepoteza mtoto mmoja.
0 comments:
Post a Comment