JUMLA YA SHILINGI BILIONI 13 KUTUMIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA!!

Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selina Kombani.

Waziri wa serikali za mitaa na Tawala za mikoa (TAMISEMI) Mh. Selina Kombani amesema uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa nchi nzima utagharimu jumla ya shilingi bilioni 13 fedha ambazo zimetengwa na serikali ili kugharamia mahitaji yote ya uchaguzi huo.
Waziri Kombani ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Wizarani hapo, amesema jumla ya vituo vya kupigia kura 60.359 vimetengwa katika maeneo mablimbali nchi nzima, katika utaratibu wa kupiga kura amesema kwa wapiga kura wa vijijini masanduku manne yatatumika katika kuwachagua wagombea kwa kila kituo na maeneo ya miji na majiji ni masanduku 3 yatatumika kuwachagua wagombea kwa kila kituo.
Kwa upande wa vijijini kutakuwa na masanduku ya kuwachagua mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa kitongoji, wajumbe wa serikali ya kijiji mchanganyiko na wajumbe wa serikali ya kijiji kwa upande wa wanawake.
Kwa upande wa miji na majiji kutakuwa na sanduku la kuwachagua mwenyekiti wa serikli ya mtaa, wajumbe wa serikali mchanganyiko na wajumbe wa serikali kwa upande wa wanawake, waziri huyo ameongeza kuwa masanduku 180.000 yako tayari na yameshasambazwa katika mikoa ya kanda ya ziwa wakati kazi ya kutengeneza masanduku yaliyosalia inaendelea.
Mh. Selina Kombani amemalizia kwa kusema uandikiswaji wa wapiga kura utafanyika kwa muda wa wiki moja na baada ya kamaliza zoezi la kuandikisha wapiga kura litafuatia zoezi la kampeni kwa wagombea ambalo nalo litachukua wiki moja na kumalizia na uchaguzi hiyo Oktoba 25 mwaka huu nchini kote

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment