Shindano bora katika afrika na lenye zawadi kubwa la Kisura wa Afrika Face Of Africa lilizinduliwa jana pale Shorpers Plaza ambapo mchakato wa kutafuta warembo watakaoshiriki katika shindano hilo utaanza hivi karibuni na kushirikisha nchi 14 za Afrika ,ambapo fainali zake zitafanyika nchini Nigeria mwezi februari mwaka 2010 na mshindi atajinyakulia kitita cha Dola za Kimarekani 50.000.
Meneja Masoko wa Maultchoice Tanzania Furaha Samalu kushoto akiceza muziki na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo jana.
Hapa Mwanamuziki Sara akitumbuiza wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa Kisura wa Afrika (Face of Africa) jana pale Shorpers Plaza jana.
Mkurugenzi wa Benchmark Production Ritah Paulsen kulia na Vodacom Miss Tanzania 2007 Richa Adhia.
0 comments:
Post a Comment