FFU wa Ngoma Africa Band katika makamuzi AFRILU Festival!!

Ras Makunja na FFU wake Ngoma Africa Band, ijumaa , walifanikiwa kuwatia kiwewe washabiki wa muziki katika onyesho kubwa la AFRILU Festival,mjini Ludwigshaven,huko ujerumani.
FFU hao walikuwa na kazi moja tu jukwaani ambayo ilikuwa ni kushambulia kwa kutumia mdundo wao wa "Bongo Dansi", na kuhakikisha kuwa muziki wao haumuachi mtu akiwa amesimama! wazee kwa vijana! wazungu na weusi,waasia na wamanga,wake kwa waume ! muziki wa Ngoma Africa umekuwa zoa zoa !fagio la kimataifa
hebu wasikilize hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment