DUH KAZI YA LEO NI NGUMU SANA MPAKA TUZIBE HAPA!!

Mafundi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka ya jijini Dar es salaam DAWASCO wakitafakari ukukubwa wa kazi kabla ya kuanza kukarabati mtalo wa maji taka uliozibuka na kumwaga maji katika barabara ya Azikiwe jijini Dar, kumekuwepo na tatizo la mitalo mingi ya maji machafu kuharibika na kumwaga maji machafu hovyo mara kwa mara jijini, hata hivyo mamlaka hiyo imekuwa ikichelewa kuchukua hatua za haraka katika kutatua matatizo hayo sijui tatizo liko wapi wadau, lakini tunawapongeza kwa kushughulikia tatizo la hapo Azikiwe ila mjitahidi kukarabati na maeneo mengine mara yanapotokea matatizo kama hayo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment