
Mkurugenzi wa Maduka ya Biggy Respect Bw.Ahmed Idd maarufu kama Biggy akiwa ofisini kwake wakati FULLSHANGWE ilipomtembelea dukani kwake Kariakoo ili kujionea kazi nzuri anayoifanya juu ya ubunifu wa nguo mbalimbali zikiwemo fulana ambazo amekuwa akizichapisha kwa maneno ya Kiswahili na kuwa kivutio kikubwa kwa vijana na watu mbalimbali wanokwenda kununua nguo hizo na kuzivaa Biggy amesema hivi sasa wameanza kupata masoko hata nchi za Ulaya na Marekani ambako watanzania wanaoishi huko wamekuwa wakiagiza ili wapelekewe huko.


Hapa kama walivyokutwa wateja wa lika mbalimbali wakinunua fulana katika duka la Biggy Respect ambalo wamiliki wake wamebuni fulana zinazochapishwa kwa maneno ya kiswahili ambazo kwa sasa zimeanza kuuzwa hata watanzania waoko katika mataifa ya Ulaya na Marekani.
0 comments:
Post a Comment