NANI ATAPIGA HATUA KATIKA ELIMU MASKINI NA TAJIRI!!

Huu ni usafiri wa wanafunzi katika mataifa mbalimbali yaliyoendelea na masikini hebu fikiria mdau ni wanafunzi gani wataweza kuendana na utandawazi na Teknolojia, kutokana na uboreshaji wa miundombinu ya kielimu katika mataifa yao jamani tutabaki tunaimba sana juu ya kuboresha elimu yetu lakini kama hatukusimama kidete kwa pamoja katika kuhakikisha kila mtu anawajibika kwa wakati wake na nafasi yake juu ya kuboresha elimu yetu hatuwezi kwenda popote.
Usafiri wa wanafunzi katika taifa letu ni moja ya vikwazo vikuu vya elimu hasa katika jiji la Dar es alaam ambapo wanafunzi wamekuwa wakinyanyaswa na kufanyiwa vitendo viovu na makondakta, mara wanapotaka kupanda katika mabasi yao wakati ama wanakwenda shule au wanarejea majumbani, kwa mtu yeyote mwenye watoto na mwenye uchungu lazima utajisikia vibaya kutokana na vitendo hivyo na utawaonea huruma watoto kutokana na matatizo haya ya usafiri kwa wanafunzi.
Watanzania wote kwa pamoja tuwajibike na kukemea kwa hili jamani ili watoto wetu wasinyanyaswe kwenye haya mabasi, lakini pia tunahitajika kufanya kazi kwa nguvu zote bila kujali huyu ni nani na huyu ana cheo gani, tufanye kazi kwa moyo mmoja na kujituma katika kuboresha uchumi wa Taifa letu ili mambo kama haya ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu yetu uwe katika uwezo wa serikali hebu, angalia kwa makini hizi picha za mabasi ya wanafunzi huenda ukawa na maoni usisite kututumia.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment