KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA SASATEL YAENDELEA KUVUNA WATEJA SABASABA!!

Mkuu wa Uzalishaji na Huduma wa kampuni ya Sasatel Thomas Andre kushoto na Meneja Masoko na Bidhaa wa kampuni hiyo bw. Derick Byarugaba aliyeshika kifurushi wakitoa vifaa mbalimbali vya mawasiliano vinavyouzwa na kuonyeshwa na kampuni hiyo katika banda lao kwenye maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya mawalimu J.K.Nyerere viwanja Barabara ya Kirwa leo tarehe 7/72009 ndiyo kilele cha maonyesho hayo ambayo yanatarajiwa kufikia tamati kesho tarehe 8/7/2009 huku Sasatel ikiendelea kuvuna wateja wa kutosha waliojiunga na mtandao huo.
Meneja wa Sasatel Tawi la Jamhuri Lusako Owen kati na Erick Kasanda msimamizi wa maduka ya Sasatel wakitoa maelezo kwa wateja mbalimbali wanaotembelea kwenye banda hilo ili kupata huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiunga na mtandao huo unaokuja kwa kasi katika mawasiliano nchini.

Watu mbalimbali wakipita katika banda la kampuni mya ya simu za mkononi ya Sasatel kwenye maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba kwenye viwanja vya mwalimu J.K Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es alaam, leo tarehe 7/7/2009 ndiyo kilele cha maonyesho haya.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment