
Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakicheza kwa staili ya kusugua kisigino katika viwanja vya Biafra kinondoni wakati wa bonanza lililoanzishwa katika viwanja hivyo na kampuni ya bia ya TBL kupitia kilaji cha Kilimanjaro Lager, baada ya kuhama kutoka kwenye viwanja vya Leaders ambako lilikuwa likifanyika kwa muda mrefu kutokana na kulifunga eneo hilo kwa ajili ya kuliendeleza Twanga walizindua albam yao hivi karibuni kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na kutikisa sana na rapa yao hiyo mpya inayowafanya watu kusugua visigino vyao bila kupenda. ilimradi shangwe tu.

Marapa wa African Satars Band Harid Chokoraa kulia na Msafiri Diof wakionyesha uwezo wao wakati bendi hiyo ilipofanya onyesho la kukata na shoka katika viwanja vya Biafra kinondoni jioni hii katika Bonanza lililoanzisha hapo na kampuni ya Bia TBL baada ya Viwanja vvya Leaders kufungwa rasmi.

Rapa wa Bendi ya African Stars Msafiri Diof kama kawaida yake akighani kwa madaha jukwaani

Mwanamuziki wa African Stars Charles Baba akiongoza mashambulizi ya wanatwanga pepeta katika bonanza lililofanyika Leaders jioni hii ni kiwanja kipya laikini kilikuwa na Burudani ila TBL wanatakiwa kuongeza ulinzi ili kuwa na usalama zaidi hasa wakati wa kumalizia bonaza hilo.

Katika vyombo vya kupuliza kwa mdomo kuna Hamis Muyupe kulia Trumpet, Shaban Redi Saxaohone kati na kushoto ni mtu mzima Roman Mg'ande akipuliza Saxaphone pia.

Wana wa Msondo ngoma ya ukae wakifanya mambo makubwa katika viwanja vya Leaders kutoka kulia ni Papa Upanga, Musemba, maalim Gurumo mzee wa kazi na Hamis Buyungwa kwenye Tumba.

Halima Bonge kimwana wa Twanga aliyestaafu akiwa na rafiki yake katika bonanza hilo ilikuwa bomba mdau japokuwa leo ilikuwa ni mara ya kwanza laikini burudani na shangwe zilikluwepo kama kawa.

Mashabiki mbalimbali wakiwa katika viwanja vya Biafra kwenye Bonanza lililoanzishwa hapo na TBL baada ya kuhamishwa kutoka viwanja vya Leaders leo kama kwaida Twanga na Msondo walikamua vilivyo katika viwanja hivyo.
0 comments:
Post a Comment