Kundi linalopiga muziki wa kisasa wa bendi kwa kutumia vifaa asilia linalojulikana kama IFA SOUND BAND liko jijini kwa maonyesho kadhaa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es alaam.
Akizungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE kiongozi wa kundi hilo Selemani Makwati ambaye pia anapiga (Drum) ngoma katika bendi hiyo amesema makazi yao ni Mkoani Morgoro katika Wilaya ya Ifakara na walikuja hapa jijini miezi mitano iliyopita kwa ajili ya kufanya maonyesho na kutafuta Riziki huku wakitafuta wafadhili kwa ajili ya kununulia Vyombo vya muziki vya kisasa.
Amesema kwa sasa wanaishi kule Mburahati Wilaya ya Kinondoni na kutembea maeneo mbalimbali ya jiji kwa ajili ya kufanya maonyesho yao ambayo watu na mashabiki wao wameonyesha kuyakubali sana ila tatizo ni Vyombo vya muziki ili waweze kwenda na wakati.
Ameongeza kuwa wao huwa wanapofika mahali fulani hupiga muziki na watu kutoa chochote na ndiyo unaokuwa ujira wao, pia anasema huwa wanaweza kupiga nyimbo za wanamuziki mbalimbali wa hapa nchini za zamani na za sasa kama vile nyimbo za FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta, Moro Jazz na bendi nyingine nyingi
Amesema pia wanazo nyimbo nyingi walizotunga anaseama "kwa mfano wimbo wetu ambao watu wengi wanaupenda unahusu kampeni ya Maralia unaoitwa (Maralia Inaua) huu wimbo umesaidia sana kuelimisha watu katika kampeni za kupambana na Maralia hasa Wilayani Ifakara ambako haswa ndiyo tunakotokea".
Kundi hili linaundwa na wanamuzikisita ambao ni Selemani Makwati (Drum) ngoma, Oswald Damka Tumba, Jafari Ligomba Gitaa la Solo, Adam Komba Gitaa la Bezi na wacheza (show) wanenguaji Chande Chilowile na Majuto Mdodo Yeyote mwenye uwezo wa kuwasaidia atuone FULLSHANGWE Tumwelekeze jinsi ya kuwapata.
1 comments:
Wana wa pakaya.Kwa hakika wanastahili kuungwa mkono.Sasa Mheshimiwa,ni vema hawa jamaa wangesema wanahitaji msaada wa aina gani.Wafikishie salamu kuwa pia tunawashukuru kwa kutangaza jina la Ifakara!
Post a Comment