KIKUNDI kinachoongoza kwa kutoa burudani kabambe ya sarakasi barani Afrika kinachojulikana kama Sarakasi Mama Afrika, juzi usiku kilikonga nyoyo za mashabiki kwenye ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam.
Mamia ya mashabiki walioingia ukumbini hapo, walishuhudia onyesho hilo la sarakasi lililoonekana kuwasisimua, huku wakifaidi uhondo huo kwa muda wa nusu saa, hali iliyosababisha baadhi yao kuwatuza pesa wacheza sarakasi hao wakiwa jukwaani.
. Mkurugenzi na mwandaaji wa maonyesho ya Sarakasi Mama Afrika, Winston Ruddle kutoka Zimbabwe, alisema maonyesho rasmi ya sarakasi ya kikundi hicho yanatarajiwa kuanza kurindima kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu eneo la Mnazi Mmoja, Dar es Salaam Mei 27, na yataendelea kuoneshwa hadi Juni 28, mwaka huu.
Katika maonyesho hayo ya Kidongo Chekundu, tiketi zitauzwa kwa sh. 16,000 viti vyekundu, sh. 12,000 viti vya bluu na sh. 8,000 viti vya kijani kuanzia Jumanne hadi Alhamisi, na watoto walio chini ya umri wa miaka 12 watalipa nusu ya gharama kwa viti vyote.
Kuanzia Ijumaa hadi Jumapili, tiketi zitauzwa kwa sh. 20,000 viti vyekundu, sh. 16,000 viti vya bluu na sh. 10,000 viti vya kijani, na watoto walio chini ya umri wa miaka 12 watalipa nusu ya gharama kwa viti vyote.
Winston alisema kila Jumanne hadi Ijumaa kutakuwa na shoo moja itakayoanza saa 1.30 usiku na itadumu kwa muda wa saa mbili na nusu; Jumamosi kutakuwa na shoo mbili zitakazoanza saa 9.00 alasiri na saa 1.30 usiku, na Jumapili pia kutakuwa na shoo mbili zitakazoanza saa 8.00 mchana na saa 12.30 jioni.
Alisema wametoa ofa ya usiku wa familia kila Alhamisi ambapo watu wazima wawili watalipa na watoto wawili walio chini ya umri wa miaka 12 wataingia bure, na akabainisha kwamba shoo za wikiendi zote zitaambatana na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakaotangazwa baadaye.
Mkurugenzi huyo alisema shule zimepewa ofa ya kuweka oda ya kuona maonyesho hayo kwa bei maalumu ya sh. 5,000 kwa mwanafunzi na akatoa mwito kwa watu kutoa oda ya sherehe na hafla mbalimbali katika hema hilo la sarakasi.
Maonyesho hayo pia yanaambatana na huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni, sherehe za shule, sherehe za kuzaliwa, sherehe za harusi, sherehe za kampuni, sherehe za makanisa na mikutano.
Vijana 65 wanaounda kundi la Sarakasi Mama Afrika, ambao wengi wao wanatoka Tanzania, wamepata mafunzo ya kutosha ya kuonesha vipaji vyao, ambavyo Watanzania wengi wanavyo.
Kikundi hicho kilichoundwa mwaka 2001 kina wasanii kutoka Afrika Kusini, Kenya na Ethiopia ambao huonyesha vionjo mbalimbali na vikaragosi, mazingaombwe na mavazi zaidi ya 500 ya kitamaduni kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

0 comments:
Post a Comment