MULTCHOICE KUONYESHA MICHUANO YA KOMBEA LA MABARA AFRIKA KUSINI!!

Meneja muu wa Multchoice Peter Fauel akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali na waandishi wa habari waliohudhuria katika hafla ya kutangaza punguzo maalum kwa wateja wake na watu wanaohitaji kuunganishiwa huduma za Multchoice na kutangaza DSTV kurusha moja kwa moja michezo ya mpira wa miguu kombe la Mabara yaani (Confedertion Cup) inayoanza kutimua vumbi juni 14 nchini Afrika Kusini na kufanyika kwa wiki mbili mfurulizo, ameongeza kuwa pia wataonyesha michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani wakionyesha michezo yote itakayochezwa katika mashindano hayo.
Ameongeza kuwa kwa watu watakaokuwa na Dishi watauziwa King'amuzi kwa shilingi 79.000 tu na watakaokuwa hawana Dishi watauziwa king'amuzi na kuunganishiwa huduma za DSTV kwa shilingi 199.000 amesema Packages zitakuwa kama ifuatavyo ambapo Family itakuwa Dola 19 kwa mwezi , Compact itakuwa Dola 25 kwa mwezi na Premium itakuwa Dola 76 kwa mwezi, hafla hiyo imefanyika leo asubuhi kwenye Hoteli ya Couryard Upanga jijini Dar.
Richard kushoto na Ray wakipeana michapo kama unavyowaona sijui wanajadili nini ah!, hata hivyo hebu tuwaache manake wanayo mengi ya kuwafanyia watanzania katika nyanja ya Sanaa na Burudani hivyo wanahitaji kupanga mikakati eti.

Meneja masoko na Mauzo wa TBC John Mbelle akisalimiana na Furaha Samalu Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania wakati wa hafla ya kutangaza ofa maalum ya watumiaji wa Ving'amuzi na wanaohitaji kuunganishiwa katia Hoteli ya Courtyard Upanga jijini leo asubuhi kulia ni mpiganaji Deus Mhagale kutoka Magazeti ya New Habari Cooparation.


Meneja mkuu wa Multchoice Tanzania Peter Fauel kulia na Meneja Mauzo na Masoko wa Africa Media GroupResty Ngonyani wakibadilishana mawazo wakati uzinduzi wa Ofa maalum ya Ving'amuzi iliyotolewa na Multchoice kwa wateja wake na watu wanaotaka kuunganishiwa huduma hiyo.
Hapa ni Richard kushoto, Mwanamuziki Witness na Raymond Kigosi (Ray) mwigizaji mahiri wa Filamu za kiswahili ambaye tayari Filamu zake zinaonyeshwa katika Televisheni ya kulipia DSTV inayoonekana katia nchi zaidi ya 150 Duniani.

Meneja mkuu wa Multchoice Tanzania Bw. Peter Fauel kulia akiwa na Mshindi wa BigBrother 2007 Richard Bezuidenhout kushoto anayefuatia kutoka kwa Richard ni Meneja Huduma Multchoice Ronard Shelukindo na Katibu Muhtasi Levina Bandiai hii ilikuwa katika uzinduzi wa ofa maalum iliyotolewa kwa wateja wanaotumia Ving'amuzi vya Multchoice kwenye Hoteli ya Courtyard leo asubuhi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment