Hawa ndiyo wanakamati wa maandalizi ya mashindano hayo kutoka Bo
Kampuni ya Bongo5 ambayo ndiyo itaandaa mashindano ya urembo katika vitongoji vya Ukonga na Kigamboni leo imefanya mkutano na waandishim wa habari katika Mgahawa wa Hadees Fast Food jijini Dar na kutangaza tarehe ambazo mashindano hayo yatafanyika katika vitongoji vyote viwili.

Akizungumza katika mkutano huo mmoja wa waratibu wa mashindano hayo Saraphia Shirima amesema tarehe hizo ni katika kitongoji cha ukonga shindano hilo litafayika Ijumaa ya Mei 29 2009 katika ukumbi wa Hill Tech Resort na kufuatiwa na Miss Kigamboni ambayo iatafanyika Mei 30 2009 katika ufukwe wa Maese Beach Resort zamani Hunters Beach Kigamboni.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yanadhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom na kampuni ya Bia nchini TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, ameongeza kuwa burudani katika mashindano hayo zitaletwa na Mwasiti, Marlow Maunda, Barnaba na Pipi kwa kushirikiana na Odama Band amemalizia kuwa fomu zinaendelea kutolewa kwa warembo wanaohitaji kushiriki katika vitongoji hivyo katika vituo vifuatavy ambavyo ni ofisi za Bongo5 zilizopo Posta mtaa wa Jamhuri Plot namba 173/3 makabala na Mkapa Tower na vilevile kupitia mtanadao wa www.bongo5.com.
0 comments:
Post a Comment