DR. HARRISON MWAKYEMBE AHAMISHIWA MUHIMBILI!!


Mbunge wa kyera mjini Dr. Harrison mwakyembe amehamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Iringa baada ya kupata ajali mbaya ya gari iliyotokea eneo la Ihemi mkoani Iringa Baada amesema mmoja wa wanahabari ambaye yuko mkoani Iringa.

Dr. Mwakyembe alikuwa akitokea Mbeya kwenda Dar es alaam katika shughuli zake za kawaida za kuhudumia jamii na taifa kwa ujumla, ameongeza kuwa Ndege maalum ya Serikali iliyomchukua kutoka Mkoani Iringa imeondoka muda mchache uliopita hivyo inaweza kuwasili wakati wowote jijini Dar kuanzia sasa ili kumpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment