TWANGA KUCHEZA MPIRA NA KUPEPETA BAGAMOYO!!

Twanga wakipepeta

BENDI ya muziki wa dansi ya The African Stars (Twanga Pepeta
International), leo (Ijumaa, Aprili 10, 2009) inatarajia kufanya
onyesho maalumu la kutambulisha nyimbo zake saba mpya katika ukumbi wa
Sadani Highway Pug.
Rapa mahiri wa Twanga Pepeta inayodhaminiwa na Zain Tanzania, Khalid Chuma 'Chokoraa' alisema Dar es Salaam jana kuwa onyesho hilo pia ni mahsusi baada ya wapenzi wa Bagamoyo kuomba bendi ya Twanga Pepeta kufanya onyesho ukumbini hapo ili waweze kupata kuiona staili yao mpya inayotesa ya 'Sugua kisigino'. Alisema nyimbo zinazotarajiwa kutambulishwa leo ni Sumu ya Mapenzi
aliotunga yeye, Mwisho wa ubaya ni aibu uliotungwa na Saulo John
'Ferguson', Sintopenda tena uliotungwa na Saleh Kupaza, Shida Darasa na
Mwana Dar es Salaam zilizotungwa na Charles Gabriel 'Chalz Baba', Nazi
haivunji Jiwe uliotungwa na Thabit Abdul na wimbo mwingine uliotungwa
na Rogart Hega 'Katapila' ambao bado haujapewa jina. Twanga Pepeta inayojiwinda na uzinduzi wa albamu yake ya kumi
unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, wanatarajia kufanya shoo kabambe ili
kuweza kukonga nyoyo za mashabiki wake watakaohudhuria leo.
Chokoraa alisema kabla ya kupanda jukwaani usiku, wanamuziki wa bendi
hiyo mchana watajitupa uwanjani kucheza mechi ya mpira wa miguu dhidi
ya Sadani ya Bagamoyo.
Alisema mechi hiyo itaanza kurindima saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa
Mwanakalenge, na akatamba kuwa Twanga FC itaibuka na ushindi kisha
usiku kuwapa mashabiki burudani maridhawa. Jumamosi Twanga Pepeta inatarajia kutumbuiza Mango Garden, Kinondoni,
Jumapili mchana wanataraji kukamua Leaders Club na usiku watakuwa klabu
ya TCC Chang'ombe.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Wacheza shoo wazuri lakini wanajiharibu na mikorogo yao na kuvaa ma wigi, wengine waonekane kama wazungu wengine kama waarabu na wahindi, hata hawapendezi mimi sifagilii kabisa mwanamke kama hivyo.

Post a Comment