PATA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI KILI MUSIC AWARD NA KITUKO CHA CHE. MUNDUGWAO!!

Hiki kilikuwa ni kituko cha mwanamuziki anayepiga muziki asilia wa Tanzania Che Mundugwao ambaye baada ya kupokea tuzo yake ya wimbo bora wa asili ya Tanzania iliyokwenda kwa wimbo Deladela uliotungwa na mwanamuziki huyo alielekea eneo la kupigia picha na baada ya kupiga picha aliiweka tuzo yake chini na kuanza kuibusu kuonyesha furaha isiyo kifani kwake Chemundugwao alitoa wito kwa serikali kuweka utaratibu mzuri na kuheshimu nyimbo za asili kwani ndiyo nyimbo pekee ambazo unaweza kuuza kwa fedha za kigeni kama ilivyo kwa wanamuziki wa mataifa mbalimbali hasa Afrika Magharibi na kusini ambao wamefanikiwa sana kutokana na muziki wa asili ya nchi zao mdau matukio katika picha ni mengi hebu shuka chini upate kuja kilichojiri katika hafla hiyo ya utoaji wa Tuzo za Kili Music Award 2009.
Nemless kutoka Kenya pamoja na kupata tuzo naye aligawa zawadi ya Burudani kwa watanzania mashabiki wake ilikuwa ni bomba sana mdau.

TOP in Dar TID akiwapagawisha mashabiki wakati alipofanya vitu vya kukata na shoka huku mashabiki wakionekana wenye furaha.

Waganda Blue3 wakifanya mambo makubwa jukwaani hebu cheki mwenyewe mdau hizo staili zao.
Keysha akinyamazishwa na ndugu zake baada ya kuangua kilio cha furaha kutokana na kushinda tuzo hiyo ya mwimbaji bora wa kike.

Mwanamuziki Keysha kusho toakipokea Tuzo yake ya mwimbaji bora wa kike kutoka kwa Sylivia mkuu wa uhusiano Mamlaka ya Elimu Tanzania.

Mkurugenzi wa Zizzou Fashion Bw. Tippo ambaye pia ni Meneja wa mwanamuziki Mangweair akipozi kwa picha na mkurugenzi wa Tovuti ya Bongo5 Bw. Lucas mara baada ya kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya mwanamuziki huyo Mangweair ameshinda kama masanii bora wa kiume.

Andrew Sekidia kulia mpiga kinanda wa Akundo Impack akipokea tuzo yao ambapo tuzo ya albam bora ya kiswahili imeenda kwa bendi ya Akudo Impact.

Meneja uhusiano wa Starndard Chatered Bank Hoyce Temu akimkabidhi tuzo Mwanamuziki Nemless kutoka Kenya ambaye wimbo wake wa Salary umeshinda Afrika Mashariki.

Hamie B. akipokea tuzo yake ya mtayarishaji bora wa nyimbo kutoka kwa Ilunga wa kampuni ya Push kushoto ni mwanamuziki AY.

QJ na Makamua wakiwa na tuzo yao ya wimbo bora wa R&B, wimbo wao wa Natamani umeshinda katika tuzo hiyo amabo wamemshirikisha Joslin aliyeko kulia.

Mwanamuziki Chid Benz akiwa ameshikilia Tuzo yake aliyoshinda kama masanii bora wa kiume mara baada ya kukabidhi wa na mwanamuziki Chingy kutoka Marekani huku mwanamuziki huyo akipungia mkono mashabiki.

Wabunifu Khadija Mwanamboka na Ally Remtullah wakiwa na Nancy Sumari kati aliyewahi kuwa Miss Tanzania.

Mwanamuziki Chipukizi Angeris kutoka pande za Arusha anayekuja juu kwa sasa akifuatilia kila kilchoendelea ili kujua atoke vipi katika tuzo zinazokuja.

Wanamuziki AY wa Tanzania kulia na Nemless kutoka Kenya wakiwa katika pozi

Vigogo wa kamati ya Miss Tanzania kutoka kulia ni Hashim Lundenga mkurugenzi, Albert Makoye mkuu wa Itifaki na Bosco Majaliwa katibu mkuu wakiteta jambo pengine ni mkakati wa jinsi ya kupiga bao katika shindano lao la Miss Tanzania mwaka huu 2009 linalotarajiwa kufanyika hapo baadae.

John Muhina kushoto ambaye ndiyo mwenyekiti wa Kili Music Award na John Dilinga mmoja wa wajumbe wa Tuzo hizo

Mbunifu wa mavazi Asia Idarous na rafiki yake Saada nao hawakuwa nyuma kujua kinachoendelea usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee katika utoaji wa tuzo za Kili Music Award 2009.

Richard Shelukindo na wenzake kutoka Multchoice wakifuatilia kwa karibu utoaji wa Tuzo hizo.

Kutoka kushoto ni wakurugenzi wa bendi ya African Stars Baraka Msirwa, Asha Baraka wakiwa na Mwanamama wa shoka Saida Simba Kilumanga.

Mrisho Mpoto akitafuta nauli ya kwenda kwa mjomba kwa kasi aliyonayo katika kutafuta lazima ataipata tu, na atakwenda kumuona mjomba huko aliko.

Wanenguaji wa Bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) wakitoa burudani ya kukata na shoka jukwaani

Keysha akipagawisha mashabiki kabla ya kutunukiwa tuzo yake ya mwimbaji bora wa kike.
Banana Zorro na kundi B. Band walifanya vitu vyao kabla ya kuanza kutolewa Tuzo za Kili.

Wanamuziki kutoka Uganda Blue3 wakihojiwa na mtangazaji wa Television ya EATV wasanii hao walifanya onyesho katika tuzo za Kili Music Award jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Kurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akiingia katika ukumbi wa Diamond Jubilee akiwa ameongozana na meneja uhusiano wa Benki ya Starndard Chartered Hoyce Temu na wagini wengine

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment