Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Uzinduzi wa kamati ya Ushauri wa Madini katika Ukumbi wa Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam kamati hiyo itakuwa na kazi ya kumshauri waziri katika masuala yote yaliyoainishwa kwenye sheria ya madini mfano uingiaji mikataba na uendelezaji madini (MDAs) na yanayohusiana na usimamizi wa sheria ya madini ya mwaka 1998.
Wanaounda kamati hiyo ni mwenyekiti Meja Jen. G. Mang'enya jaji mstaafu mahakama ya kijeshi wajumbeni Bw. Erick Mugurusi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Bw Joseph Stanley Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dr. Philip Mpango Wizara ya fedha na Uchumi, Bi. Maria Kejo Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali, Richard Kasesela Sekta Binafsi na Mh. Esther K. Nyawazwa (Mbunge) kutoka sekta binafsi ambapo mwakilishi kutoka Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko bado hajateuliwa.
0 comments:
Post a Comment