Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera akizungumza wakati alipozindua rasmi nembo itakayotumiwa katika mashindano ya Vodacom Dar es alaam International Marathon yatakayoanza kutimua vumbi kwa mara ya kwanza juni 21 mwaka huu, katika mashindano hayo kutakuwa na mbio za km5 Vodacom Fun Run na km21 na watakaoruhusiwa kukimbia mbio ndefu ni kuanzia miaka 18 isipokuwa mbio za km5 wanaweza kushiriki watu mbalimbali katika udhamini huo Vodacom imetoa jumla ya shilingi milioni 50 ili kufanikisha mbio hizo
Mkurugenzi wa masoko Vodacom Efraim Mafuru akimkaribisha Mh. Naibu waziri Joel Bendera ili aweze kuzungumza na kuzindua rasmi nembo ya mashindano ya riadha ya Vodacom Dar es alam International Marathon yanayotarajiwa kufanyika juni 21 mwaka huu jijini Dar.
Katibu mkuu wa Olimpiki Tanzania Filbert Bayi akiwashukuru Vodaco m kwa kuanzisha mashindano ya Riadha Vodacom Dar es Alaam International Marathon wanaofuatia katika picha ni katibu wa chama cha riadha Suleiman Nyambui Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Rwehumbiza Meneja udhamini na mawasiliano Vodacom na Efraim Mafuru mkurugenzi wa masoko Vodacom kampuni hiyo imetoa Zaidi ya shilingi Milioni 50 kafanikisha mashindano hayo.
Naibu waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mh Joel Bendera kulia pamoja na Meneja udhamini na Mawasiliano wa Vodacom George Rwehumbiza wakionyesha nembo ya mashindano mapaya ya Radha yaliyoanzishwa yatakayojulikana kama Vodacom Dar es alaam International Marathon yatakayofanyika kwa mara ya kwanza tarehe 21 juni mwaka huu hapa jijini kushoto ni mkurugenzi wa masoko Vodacom Efraim Mafuru na kulia mwisho ni katibu wa olimpiki Filbert Bay na Suleiman Nyambui katibu wa RT.
0 comments:
Post a Comment