PATA MATUKIO YA ONYESHO LA FATMA AMOUR (KAKAKUONA) KATIKA PICHA!!

Fatma Amour mwenye nguo nyeusi akiwa pamoja na wanamitindo walioonyesha nguo zake mara baada ya onyesho lake lililojulikana kama Kakakuona Unavyovaa Ndivyo ulivyo ambalo limefanyka usiku wa kuamkia leo kwenye ufukwe Dar Alive akribu kabisa na Cine Club jijini kwakweli lilikuwa ni onyesho la kusisimua kutokana na ubunifu ulioonyeshwa na wabunifu walioonyesha nguo zao kwa matukio zaidi katika picha shuka chini upate kujua kilichojiri katika onyesho hilo mdau.
Hapa wanamitindo wakipita na nguo zilizobuniwa kwa nguo na ngozi hayo ndiyo mambo ya kakakuona.
Kulia Fatma Amour, Matukio Chuma, Robby Morro mamaa wa Mapozi na Franco wakipozi kwenye Camera ya FULLSHANGWE.
Hapa ni wabunifu Zamda George kulia mbunifu chipukizi aliyefanya vizuri sana katika onyesho la Lady in Red lililofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski likiandaliwa na Asia Idarous hivi karibuni wengine ni Mamaa Franco kati na Farha.
kulikuwa na wabunifu wengi waliojitokeza kushuhudia onyesho hilo kama unavyoona hawa kutoka kulia mamaa Frasisca Shirima aka (Franco)mbunifu wa siku nyingi huyu katikati Farha na mkongwe Khadija Mwanamboka.
Mbunifu Mustaffa Hassanali akampiga tafu Fatma Amour kama wanavyoonekana kupozi mbele ya Camera ya FULLSHANGWE mara baada ya onyesho hilo.

Mwanamitindo huyu alivutia sana na vazi lake huku akiwa ameshikilia kibuyu na simu yake kweli hili lilikuwa onyesho la Kakakuona wadau.
jamani vibuyu kumbe ni urembo katika nguo pia.


Kama unavyoona mdau mavazi haya yamebuniwa kwa kuchanganya vitu vingi vya kiasili vikiwemo vibuyu.
Hii ilikuwa ni moja ya nguo maalum kwa wakina mama wajawazito zilizoonyesha katika onysho hilo.
Haya ni miongoni mwa mavazi yaliyoonyesha jana yakiwa yamebuniwa na Fatma Amour, mavazi haya yamebuniwa kwa mfano wa wanyama mbalimbali kama vile Tembo, Faru, Nyati, Nyoka na wengineo.

Ikafika zamu ya kuona mambo yenyewe ya kakakuona yaliyoletwa na mbunifu Fatma Amour.

Hapa Angeris akikamua Vya kutosha mbele ya mashabiki waliohudhuria katika onyesho hilo lililofanyika ufukwe wa Dar Alive jijini karbu na Cine Club.
Msanii Angeris na ye akafanya mambo makubwa katika onyesho hilo na wimbo zake My Boo
Gabriel Saktamole akiwa na wanamitindo walioonyesha nguozake katika onyesho la Kaka Kuona.






Wanamitindo wa kimasai wakiwa katika mavazi yaliyobuniwa na mbunifu Gabriel Saktamole kulia

Baadhi ya wanamitindo wakiwa katika mavazi yaliyobuniwa na mbunifu Las Mizizi


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

3 comments:

  1. full shwangwe kweliwkeli DHUUUUUUUUUU!!!! huyu fatma ni mmbunifu kweli kweli haijapata kuonekana katika wabunifu wote tanzania!!! yaaani wee achatu dada fatma upo juu umefunika kichizi sio mchezo dada... kila la kheri ..

  2. sijaona zaidi ya ubunifu wa mitungi na vibuyo umeniwacha hoi hongera sana dada fatma amour upo juu tuna kupa moyo uendelee na kazi zako tunakuaminia .....

  3. kakakuona kaonekana daralive!

Post a Comment