Kocha Marcio Maximomwenye suti nyeusi akiwa na baadhi ya waandishi na mashabiki wa timu hiyo wakati ilipowasili jana kwenye uwanja wa ndege wa kimatifa Julius K. Nyerere
Sisi FULLSHANGWE tunakupa heko sana kocha Marcio Maximo kwa kutokubali kuyumba
katika misimamo yako na maamuzi yako mbalimbali ambayo umekuwa ukiyatoa na kuyasimamia kwani tumeshuhudia makocha wengi wenye kusikiliza kila jambo wakipata matatizo sana katika kazi zao kutokana na kushauriwa na watu ambao pengine hawajui mambo muhimu yanayohusu mpira ama wanafanya makusudi ili kuharibu.
Makocha wengi wanakuwa na utaratibu wao wa kufanya kazi na wanajua nini wanafanya kama alivyo Marcio Maximo ndiyo maana utakuta kwa kipindi hiki toka Maximo achukue Taifa Stars timu yetu inajaribu kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali tunayoshiriki japokuwa siyo kwa kiwango kikubwa sana ingawa ukiacha vipaji wachezaji wetu ni wa kiwango cha kawaida sana kuanzia mafunzo, ufundi katika mchezo, mbinu na Utomvu wa nidhamu ambayo ndiyo imekuwa ikilalamikiwa sana na kocha Maximo, kwani mara nyingi amekorofishana na baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars walioonyesha nidhamu mbovu katika timu hiyo kama ilivyotokea kwa Juma Kaseja na sasa Haruna Moshi na Athuman Idd.
Wadau tumuache kocha afanye kazi yake ila Tumpe ushirikiano bado tuna safari ndefu ya kutengeneza timu yenye Ushindani, Nidhamu juhudi binafsi , mbinu na mambo mengine mengi yanayohitajika ili tuwe na timu bora kama yalivyo mataifa mengine katika Afrika na kwingineko Duniani lakini tunatakiwa kuacha siasa na ubinafsi kwanza ndipo malengo yetu yatimie lakini si kwa kuongea sana wala kuandika sana kwenye makaratasi mipango isiyotekelezeka, mwenye maoni zaidi atutumie nasi tutayarusha laivu wadau.
0 comments:
Post a Comment