Msanii juma Nature aliyeshika kipaza sauti kutoka kundi la TMK Wanaume Halisi atatema chechezake leo pale atakapoanza kugawa Umasikini wake kwa mashabiki watakaofurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ili kushuhudia ugawaji huo wa umasikini uatakavyokuwa ukienda.
Juma Nature na Kundi lake linalojumuisha wasanii kibao likiongezwa nguvu na msanii JB aliyejiunga na kundi hilo kutoka Babaga Fresh na wengine kama Ferouz, Makamua na wengine wengi ni wazi kuwa shughuli yao ya leo Pale Diamond Jubilee itakuwa pevu na itapata mashabiki lukuki kama ambavyo imekuwa ikijitokeza katika maonyesha ambayo yamekuwa yakifanywa na msanii huyo kutoka Wilaya ya Temeke, wadau wote wa muziki wa Bongofleva mnakaribishwa kuja kuona mambo katika picha kushoto wanaofuatia ni Ferouz na JB.
1 comments:
hallo whow nice is ur blog out there.
i real like ur blog..
keep it up men...
welcome and follow my blog as well.
its http://samvande.blogspot.com
regards.
Post a Comment