KAMANDA KOVA AZUNGUMZIA SHAMBULIO LA RAIS MSTAAFU ALLY HASSAN MWINYI!!


Kamanda wa Kanda Maalum ya kipolisi mkoa wa Dar es alaam kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya polisi kituo cha kati wakati alipotoa taarifa juu ya mtuhumiwa Ibrahim Said Sultan maarufu kama (Ustaadh) aliyemshambulia Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi kwa kumpiga kofi wakati akitoa hotuba katika Baraza la Maulid katika ukumbi wa Diamond Jubilee Juzi Kamanda Kova amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kupima afya na akili yake pia kujua kama mtuhumiwa ni mwanaharakati na kama alikula njama na watu wengine kufanya kitendo hicho, kova ameongeza juwa mtuhumiwa amehojiwa na kueleza kuwa hakuwa na nia ya kumdhuru Rais Mstaafu huyo lakini kwa kuwa ni mtu maarufu na anapendwa na watu wengi aliona akimfanyia kituko hicho atakuwa amefikisha ujumbe wake ambapo kijana huyo anapinga waislamu na wakristo kushirikiana katika kusherehekea sikukuu zao pia hapendi viongozi wa dini kushawishi jamii kutumia kondom kwani kwa mujibu maelezo yake ni kahamasisha matendo maovu,kesho Ibrahim Sultan atafikishwa mahakama ya Kisutu kwa kujibu tuhuma zinazomkabili.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment