Wana Kalunde Said anayepiga gitaa la Sollo na Junior wakifanya mambo makubwa wakati walipowatumbuiza wageni mbalimbali katika chakula cha jioni kwenye Hoteli ya Peacock iliyopo Millenium Makumbusho jana usiku.
Hawa pia ni Harryscott Bowden, Tom Lacey na Georgia Sharp wageni kutoka Uingereza ambao wako nchini wakifanya kazi ya kujitolea kwenye kampuni ya The Leap Tanzania nao walijumuika na wenzao ili kupata shangwe za Kalunde Band na Machozi Thietre.
Kulukuwa na wageni mbalimbali kama unavyowaona kutoka kulia ni Belimda Mlingo, Ritha Mbuli na Sabrina Sampson kutoka Uingereza ambaye yuko hapa nchini kama mfanyakazi wa kujitolea katika kampuni ya The Leap Tanzania.
Nao Kalunde wakafanya mambo kama kawaida yao kama unavyowaona Debora Nyange kuanzia kulia, Rola Maganga na Said wakiwajibika kwa mashabiki wao katika onyesho lililofanyika jana kwenye chakula cha jioni Hoteli ya Peacock Millenium Makumbusho.
0 comments:
Post a Comment