Kwa mara nyingine tena mwaka huu Tanzania ilishirika katika maonyesho ya Utalii yajulikanayo kama World Travel Market (WTM) yaliyofanyika jijini London Uingereza kuanzaia 10-13 Novemba mwaka huu Maonyesho haya ni kati ya maonyesho makubwa matatu duniani na mwaka huu yalifanyika katika viwanja vya EXCEL vilivyopo jijini London.
Tanzania iliwakilishwa na ujumbe mzito kutoka Tanzania Bara na Visiwani, ujumbe huo uliongozwa na Mh. waziri wa Mali asili na Utalii Shamsa Mwangunga na taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo kama vile Bodi ya Utalii (TTB), Hifadhi ya Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA) pia wizara ya Utalii na Biashara na Uwekezaji Zanzibar, Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Tasisi zilizoko chini ya kamisheni ya Uwekezaji Zanzibar.
Pia kulikuwa na ujumbe kutoka kampuni binafsi zinazojishughulisha na biashara ya Utalii zipatazo 83 na mwandishi mmoja kutoka chombo binafsi, lakini pia kulikuwa na kundi la muziki wa asilia kutoka Tanzania lijulikanalo kama SISI TAMBALA lililokuwa na wanamuziki 8 na liliweza kuonyesha mambo makubwa katika muziki wa asili ya Tanzania ili kupata matukio mbalimbali yaliyojiri katika maonyesho hayo FULLSHANGWE inakudondoshea matukia katika picha moja kwa moja kutoka UK pata vituuuu!!
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiFyHy19BLU_0retn03C89aMPi-nq4UeWz9Vhapg-kRp7CIc8OeSkxW3L7MjEaLjPYz8YlZ3cCHCr972Y3feZlwdZj6UPJ7H_317M9xvFrbnI35KL12p3ZhHlz6r17Zw3lgYj9YNZScuyg/s400/Tambara+021.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhCfRnFFBv9wRiJLnIEQTSlP6Ej_PS2pwVWmNM9qQ2DpuSiMHZClhpyUmyn-MZsZwS-7hBx8M3zVBnvYkIxVDUQz9AbtG8hdmh6vf-MCMm_zF4zLgdIXH7kitFP2q9z2tbuCfWzIcXBcpU/s400/Tambara+020.jpg)
\
Bendi ya Kitoto yenye makazi yake nchini humo ikifanya vitu vyake katika sherehe mara baada ya maonyesho hayo kumalizika
Meneja Masoko wa bodi ya Utalii Tanzania Geofrey Meena kushoto akiwa na Juma Pinto mtanzania ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuutangaza utalii waTanzania nchini uingereza
Katibu mkuu Wizara ya maliasili na Utalii Bi. Blandina Nyoni akizungumza na mkurugenzi wa mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Peter Mwenguo katikatika wakati wa maonyesho ya Utalii nchini Uingereza kulia ni Bw. Kashangwa wa Tanzania Trade Centre nchini humo
Katibu mkuu Maliasili na Utalii Bi. Blandina Nyoni kulia na Meneja masoko wa Tanzania Tourist Board Bw. Geofrey Meena kushoto wakiwa na wadau wengine wa mambo ya utalii katika maonyesho hayo.
0 comments:
Post a Comment