ZAIN YAING`ARISHA GOFU KILOMBERO


Samson Majwala: Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Samsom Majwala akifurahia baada ya kupiga mpira na kuingia shimoni wakati wa mashindano ya gofu yaliyodhaminiwa na Zain kwenye viwanja vya gofu mjini Kilombero jana

Patti Bennie, Greg Ascough, Samson Majwala: Mshindi wa kwanza wa mashindano ya gofu ya Kilombero yaliyodhaminiwa na Zain, Patti Bennie akikabidhiwa kombe na nahodha wa klabu ya gofu ya Kilombero, Greg Ascough mjini Kilombero jana. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Samsom Majwala.

Niki Kazuka, Greg Ascough: Ofisa Mauzo wa Zain Tanzania, Niki Kazuka akichagua majina ya wachezaji walioshindana kwa makundi katika mashindano ya gofu ya Kilombero yaliyodhaminiwa na Zain mjini Kilombero jana huku akishuhudiwa na nahodha wa klabu ya gofu ya Kilombero, Greg Ascough.


Jonas Fute, Greg Ascough, Samson Majwala: Mshindi wa pili wa mashindano ya gofu ya Kilombero yaliyodhaminiwa na Zain, Jonas Fute akikabidhiwa kombe na nahodha wa klabu ya gofu ya Kilombero, Greg Ascough mjini Kilombero jana. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Kati wa Zain Tanzania, Samsom Majwala.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment