Mamillion Sauti za Busara Festival Artists 2009


style
urban / kwaito / hiphop
festivals
Sauti za Busara 2009
recordings
Phakama (2007)
Sphiwe Ngwenya, aka Mamillion hails from Soweto. He is inspired by township life, the changes of music genres and the country’s constant challenges. He aims to take kwaito back to the TKZee era with his beats, whilst fused with a modern sensibility.
Mamillion’s main objective is to entertain while dominating the kwaito scene. Mamillion is a newly signed artist to Tsotsi Taal Productions, the company that discovered Teargas who were the label's first South African hiphop act to scoop three Metro FM Awards out of four nominations.
Mamillion’s recent debut CD, Phakama is filled with party songs, tracks inspired by his social struggles and a constant ambition of making his first R 1,000,000 through music. The album also includes the bonus track “Gatvol” that directly targets taxi drivers for their controversial behaviour.
With the help of talented producers like 635 (who also produced the Teargas album including the Number 1 hit “Chance”), Mellow and B-MA, the album demonstrates how Tsotsi Taal Productions are developing and grooming young upcoming musicians and producers. The charismatic Mamillion has successfully put together an educative, motivational and entertaining album, featuring hits like Mzimba Nyakaza, Thingz Change, the controversial bonus track “Gatvol” and more.
“Mamillion added a new project to the kwaito collection last year in the form of a ten track album titled Phakama. The album features some slick joints that can drive you real mad if you have a good ear for kwaito with a touch of hip hop. Predominantly, Mamillion’s jams are for dancing but I also like the way he slows down on other tracks putting across a little subject matter. The project is charming enough to lure a multitude of youths who will find the issues of love, partying and thugin’ all packed into one offering. Like most kwaito artists, Mamillion makes sure he puts an aggressive stamp to his vibe. The title track Phakama (“Flee”) says it all – “I’m back so you better run for your life or else”. His lyrical capabilities are something many kwaito cats are struggling to develop and he truly knows how to treat the mic. A bit rough but carefully spitting out his outspoken thoughts that don’t clash with the beat like other rap upstarts often do. The sixth track, Thingz Change drops some cool sounds; I also find myself impressed with the way the instruments are arranged on this particular track. Thingz Change talks about the changing living conditions in South Africa which are increasingly becoming unbearable for the unemployed.” (excerpt from CD Review by Eddie Hatitye)

Mwanafunzi Manyara aibuka milionea wa Zain

Mratibu wa Huduma ya One Network ya Zain Tanzania, Togani
Ngotta (wa pili kushoto) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kumpata mshindi wa
pili wa fedha taslimu sh. milioni 1 wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain
Tanzania, Paul Peter wa Manyara, jijini Dar es Salaam jana (Desemba 19, 2008).
Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Zain Tanzania (Kitengo cha Wateja), Kelvin
Twissa, mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Saleh na
Ofisa Uhusiano wa Zain Tanzania, Celine Njuju.



MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Chifara iliyoko
mkoani Manyara, Paul Peter ameibuka mshindi wa sh. milioni 1 katika promosheni
yake ya Endesha Ndoto 2 kwenye droo iliyofanyika Dar eS Salaam jana.

Paul (19) ameibu mshindi ikiwa ni siku moja baada ya mkazi wa Mwanza, Wilfred
Baltari (24) kuwa mshindi wa kwanza kuibuka na sh. milioni 1, promosheni
itakayoendelea kila siku hadi Desemba 31, mwaka huu.

Mwanafunzi huyo aliibuka mshindi katika bahati nasibu iliyosimamiwa na mkaguzi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Saleh, Meneja Masoko wa
Zain Tanzania (Kitengo cha Wateja), Kelvin Twissa na Ofisa Habari wa Zain
Tanzania, Celine Njuju.

Twissa alisema Zain imeongeza zawadi za fedha taslimu katika promosheni ya
Endesha Ndoto 2 kuwawezesha wateja kufurahia msimu huu wa sikukuu za Krismasi
na Mwaka Mpya ili waweza kununua mahitaji mbalimbali.

Kushiriki katika droo ya zawadi za fedha taslimu, mteja wa Zain anapaswa kuwa
amejiunga na promosheni ya Endesha Ndoto 2 kwa kutuma neno Ndoto kwenda
100, na pia wataweza kushinda zawadi kubwa ya gari jipya aina ya Toyota Land
Cruizer na nyingine za muda wa maongezi na simu za mkononi.

Zain pia inachagua mshindi wa muda wa maongezi wa sh. 100,000 kila Alhamisi na
wateja wengine wa Zain wapatao 1,100 pia wanapata muda wa maongezi katika droo
hiyo, 100 wanapata muda wa maongezi wa sh. 25,000, na wateja 1,000 wanapata
muda wa maonegezi wa sh. 5,000 kila mmoja.

Zain imekuwa ikitoa gari moja aina ya Toyota RAV 4 kila mwezi tangu mwanzoni
mwa mwaka huu katika promosheni ya kutoa zawadi ya magari kubwa kuliko zote

katika historia ya Tanzania. Mshindi wa RAV 4 ya 10 atachaguliwa wiki ijayo
ilhalimshindi wa zawadi kubwa katika promosheni hiyo ya Toyota Land Cruiser
atachaguliwa Decemba 31 mwaka huu.

CLAUDIO NUYIMANA KUTOKA BURUNDI ANYAKUA TAJI LA MISS EAST AFRICA!!


Mshindi wa pili Annete Mwakaguo (kushoto) Miss East Africa, Claudio Nuyimana (katikati) na mshindi wa tatu, Anais Veerapatren katika shindano liliofanyika jijini Bujumbura juzi, kwa habari zaidi katika picha shuka chini.
Miss East Africa, Claudia Nuyimana akivishwa taji mara baada ya kutangazwa mshindi wa shindano lililofanyika juzi jijini Bujumbura.

Majaji wakijumlisha maksi walizopata washiriki mara baada ya washiriki wote kupita jukwaani kwa nyakati tofauti kulingana na utaratibu ulivyokuwa.

Laura grenouille na cinderela sanyu wakipitajukwaani na vazi la jioini.

Baadhi ya Warembo walioshiriki Shindano la miss East Africa wakipita jukwaani wa kwanza kutoka kushoto rahwa gjhidey, anais niragira na claudia nuyimana.

VICK ISSANJA AMEREMETA KATIKA SHEREHE YA KUMUAGA (SENDOFF)!!

Vick Issanja kushoto akiwa na Matron wake wakimeremeta vilivyo katika sherehe ya kumuaga (Sendoff) walipendeza vilivyo sherehe ilifanyika Five star hall Mbezi Beach.
Vick Issanja kushoto akimshukuru Dada yake na mama yake mlezi mamaa Mariam ambaye pia ni mkurugenzi wa maduka ya Pentagon Shoping Center jijini wakati wa sherehe ya kumuaga mdogo wake(Sendoff) iliyofanyika Five Star Hall Mbezi Beach jijini jana.


Mamaa Salma King aliyekaa kulia akiwa na wageni wengine walioalikwa katika sherehe hiyo iliyofanyika Mbezi Beach katika ukumbi wa Five Star.

Mh. Jaji Mkuu wa Tanzania Augustino Ramadhani pia alijumuika na wagemi waalikwa wengine katika Sherehe hiyo ya kumuaga Bi Vick Issanja.
Mussa Loth Abraham mkurugenzi wa Jahman Fashion mwenye suti nyekundu na kundi lake nao walijitokeza katika kuhakikisha wanamuaga Vick Issanja katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Five Star Mbezi Beach jana.


ONESHO LA MAISHA MAZURI, MUZIKI MZURI! JHIKOMAN AONGOZA MASHAMBULIZI NA KUZINDUA TUPENDANE!!

Umoja ni nguvu!Wasanii wa kitanzania wapigao muziki wenye vionjo vya kitanzania wamekonga nyoyo za wapenzi wa muziki Bagamoyo!Onyesho la pili linatajiwa kufanyika Dar es Salaam tarehe 21 Desemba nyumba ya sanaa!KIIGILIO NI BURE! hebu pata matukio katika picha jinsi onyesho hilo lilivyokuwa.
Wapenzi wa muziki wakijimwaga ukumbini.

Catherine akiimba jukwaani.


Antonia naye hakubaki nyuma katika kuonyesha uwezo wake kwa kuimba.


Ashimba & Kauzeni wanopiga muziki wa asili wakiwajibika vilivyo jukwaani.

Zain Kutengeneza milionea mmoja kila siku kwa endesha ndoto2!!.


Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe anayesomeshwa na Zain Tanzania, Noel Mazoya (wa pili kulia) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kumpata mshindi wa fedha taslimu sh. milioni 1 wa promosheni ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain Tanzania, Wilfred Baltari wa Mwanza, jijini Dar es Salaam jana (Desemba 18, 2008). Kushoto ni mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein, Meneja Masoko wa Zain Tanzania (Kitengo cha Wateja), Kelvin Twissa na kulia ni Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya.

MISS EAST AFRICA ILIFANYIKA JANA BUJUMBURA FUATILIA BLOGU HII KWA HABARI ZAIDI ZA WASHINDI!!

Rahwa Ghebrehiwet (kushoto) Mkurungezi wa Rena Events, Rena Callist ambaye ndiyo mribu wa shindano hilo na Manal Husein.
Anit's veerapatren (mauritius), Manal Hussein (eritrea), Rahwa Ghebrehiwet (eritrea), Claudia Noyimana (Burundi.


Baadhi ya warembo walioshiriki shindano la Miss East Africa lililofanyika Jijini Bujumbura Burundi Kutoka kushoto aisha Ahamed, Idimulisa Dominique, Laura Greovlle, Anats Veerpatren, Brigitte Kaneza, Rahwa Gilbert, Anois Niragira, Lucy Njambi na Sarah Mbogori.


MISS EAST AFRICA NI KESHO BUJUMBURA,WAREMBO WA TANZANIA KUVUNA NINI?

Annete john wa Tanzania katika poozi, pata matukio katika picha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Rena Events inayoaandaa shindano laMiss East Africa, Rena Callist (kushoto) akiwa na Mhariri wa Gazeti laBingwa, Petter Mwendapole (kulia) na wawakilishi wa Tanzania katikashindano hilo, Anette Mwakaguo (nyuma kushoto) na Lynnete Lwakatarewakiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bujumbura.


Baadhi ya washiriki wa shindano la Miss East Africa wakiwa katka vazi la ufukweni

Baadhi ya washiriki wa Miss East Africa wakiwa mazoezini tayarikwa fainali zitakazofanyika kesho.


Annete john kushoto akiwa na mratibu wa Miss EAC Burundi, Serge Nkurunzinza na Lynete Rwakatare.


Mwakilishi wa Tanzania, Lynnete Lwakatare akihojiwa na waandishiwa habari.

MBILIA BELL AWASILI TAYARI KUWASHA MOTO J/MAMOSI!!

Mbilia Bell akihojiwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

Mwanamuziki Mbilia bell kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo katikati akiiwasili katika uwanja wandege wa mwalimu julius kambarage Nyerere usiku wa kuamkia leo mbilia atakuwa na onyesho pamoja na Farii Ipupa kwenye viwanja vya New Word Cinema jumamosi jijini.

Kikao cha kamati cha ushirikiano kati ya JKU na JKT kuanza kesho!!


Na Anna Nkinda – Maelezo
16/12/2008 Kikao cha siku mbili cha Kamati ya ushirikiano baina ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) kwa upande wa Zanzibar kinatarajia kuanza leo (kesho) makao makuu ya JKT Mlalakuwa jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho cha siku mbili kinatarajiwa kufunguliwa na Kaimu Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Samweli Kitundu.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kinatarajia kuzungumzia jinsi ya kuimarisha ushirikiano wa jadi uliopo kati ya majeshi hayo, kutafuta nyanja mpya za ushirikiano zitakazoharakisha kukua na kuimarika kwa ushirikiano baina ya pande mbili na kuangalia maeneo ambayo kila upande utaweza kunufaika hasa upande wa kilimo na ufugaji.

Majeshi hayo yanaushirikiano wa muda mrefu tangu mwaka 1975 pale rais wa awamu ya pili wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Aboud Jumbe alipofanya ziara ndani ya JKT na kuvutiwa na majukumu ya Jeshi hilo katika malezi ya vijana ambapo alitoa msukumo wa kuanzishwa kwa kamati maalum ya ushirikiano baina ya pande mbili za Muungano.

MWANAMUZIKI ROGERS LUCAS ATATISHA NA "RUDI"!!

Rogers Lucas akiwa katika picha ya pamoja na Gwiji la muziki kutoka Paraguay Ricardo Flencha mara baada ya onyesho lao nchini Uswisi.


Rogers katikati akipiga ngoma na kuimba wakati walipokuwa jukwaani katika moja ya matamasha yaliyofanyika ulaya hivi karibuni ambapo mwanamuziki huyo kutoka Tanzania alishiriki.


Kundi la wanamuziki walioshiriki na mwanamuziki Rogers Lucas katika tamasha la muziki nchini ujerumani wakiwa katika picha ya pamoja.

Mwanamuziki chipukizi Rogers Lucas yuko mbioni kuingiza Albam yake mpya sokoni baada ya kuikamilisha kwa mafanikio huku akipata mialiko kadhaa katika nchi za Magharibi kama Ujerumani Uswisi na Australia, Albam hiyo inajulikana kwa jina la Rudi ni moja ya Albam bora zilizowahi kutolewa na wanamuziki Chipukizi katika muziki wa BongoFleva hapa nchini .

Rogers kijana anayeonekana mtulivu anayependa kutembea huku akiwa amebeba gitaa lake amekuwa akipata mialiko kadhaa hapa nchini na nje ya nchi ambapo amefanya maonyesho yake kwa mafanikio makubwa, lakini pia ameshirikiana na wanamuziki wakubwa kama vile Ricardo Flecha kutoka Paraguay Amerika ya kusini mwanamuziki ambaye anaheshimika sana katika ukanda huo kwa uwezo wake katika kupiga muziki.
Wakati Fulani niliwahi kumshuhudia Rogers ambaye ana uwezo mkubwa katika kupiga gitaa na kuimba katika onyesho moja la mavazi lililohusisha wanamitindo maarufu hapa nchini ambalo lilifanyika kwenye Hoteli ya kitalii ya Kilimanjaro Kempiski katikati ya mwaka huu alionyesha uwezo mkubwa na sauti yake ilivutia watu wengi waliohudhuria katika Onyesho hilo.

Albam ya Rogers ina nyimbo nane ambazo ni Mama, Niambie Leo, Jasho la Upendo, Ni Wewe, Si Utani, Hayupo na Rudi wimbo uliobeba jina la Albam hiyo, mpaka sasa Albam iko tayari na itakuwa madukani hivi karibuni watu wote wakae mkao wa kula na kupata burudani iliyomo ndani ya Albam hiyo.

Nawal Sauti za Busara Festival Artists 2009!!


style
acoustic / roots / fusion / spiritual
festivals
Sauti za Busara 2009
website
recordings
Kweli, 2001; Aman, 2007
Born in the Comoros islands into a family with many musicians, Nawal bathed in both popular and spiritual music from a young age, in her native islands and also in her new home in France.
Between traditional and contemporary, Nawal’s music weaves a rich dialogue of cultures, a reflection of the diverse character of life in the Comoros. Indo-Arabian-Persian music meets Bantu polyphonies, the syncopated rhythms and Sufi trance of the Indian Ocean. Nawal sings in Comoran languages, Arabic, Kiswahili, French and English.
An acoustic roots-based fusion, her music is rhythmically compelling and beautifully lyrical. Known as the “Voice of Comoros,” Nawal is also the first Comoran woman singer/songwriter and multi-instrumentalist to give performances in public. As a Muslim-born African woman who does not always adhere to traditional socio-religious codes, Nawal has faced many challenges in her career, yet she remains strong in her message and philosophy. Descending from the grand Sufi marabout of Comoros, El-Maarouf (1852-1904), Nawal invariably stays with the light of Islam founded upon love, respect and peace. In her music, she sings in favour of humanity, for education and for unity.
Nawal has gained international praise as a self-produced artist with her powerful voice and socially progressive commentary. Nawal has performed professionally for 20 years, and as a multi-instrumentalist she plays the gambusi (Comoran banjo-like instrument, cousin to the oud), the dof (Iranian frame drum) and guitar, among others.
Her first full-length album, “Kweli” (Truth), was released in 2001 and was well-received by fans and the press. Putumayo featured Nawal’s song “Hima,” recorded with Donna Africa, on the ""Women of Africa"" compilation released in 2004. Nawal always enjoys to engage herself in numerous collaborations with artists of different horizons and mediums.
It has been a dream of Nawal to visit Zanzibar since her childhood days in Comoros. Along with Nawal, performers at Sauti za Busara 2009 are as on the album, featuring Idriss Mlanao on contrabass and Melissa Cara Rigoli on mbira and percussion.
“downright gorgeous music; a record that’s going to become a long-term favourite.” Aman CD Review, Ian Anderson, fROOTS, Oct 2007
“One of the most notable world music CDs released over the last year” Jon Pareles, New York Times, June 2007

Zain yazindua huduma ya simu Ghana!!


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain Afrika, Bw. Chris Gabriel akiuza kadi ya simu kwa mteja wakati wa hafla ya Zain kuzindua huduma ya simu selula nchini Ghana, uzinduzi ulioambatana na kutoa huduma ya intaneti ya 3.5G jijini Accra, Ghana juzi.


· Yatambulisha mtandao wa intaneti wa 3.5G
· Yawekeza dola milioni 420 nchini Ghana
· Huduma ya ‘One Network’ yafikia nchi 17

Accra, Ghana – Desemba 15, 2008
ZAIN, kampuni ya simu inayoongoza kwa kutoa huduma katika nchi 22 Mashariki ya Kati na barani Afrika, imezindua huduma ya simu selula nchini Ghana, uzinduzi ulioambatana na kutoa huduma intaneti ya 3.5G kwa mara ya kwanza nje ya Afrika Kusini.
Mtandao wa Zain nchini Ghana utawawezesha wateja wake kupata huduma bora na ya haraka ya intaneti na kwa mara ya kwanza nchini Ghana watakuwa na uwezo wa kupokea simu zenye video ikiwa ni pamoja na kutuma picha za video, muziki na picha nyinginezo.
Huduma ya intaneti ya 3.5G ya Zain itawawezesha wananchi wa Ghana kuishi katika maisha mapya. Uzinduzi huo ulifanyika juzi katika mji mkuu wa Accra, na Zain imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 420 kwa ajili ya kuimarisha huduma za mtandao huo nchini Ghana.
Kutokana na uzinduzi huo, Ghana imefanya idadi ya nchi zilizojiunga katika huduma ya ‘One Network’ kufikia 17. Huduma ya ‘One Network’ ya Zain isiyo na mipaka katika simu inatumiwa na zaidi ya watu nusu bilioni Mashariki ya Kati na barani Afrika – ambalo ni eneo kubwa kuliko Marekani.

Huduma ya One Network ya Zain ndiyo kitu ambacho kinapaswa kuangaliwa kwa hali ya juu kabisa katika mageuzi ya mfumo mpya wa kampuni. Kwa uzinduzi huo, wateja wa Ghana wanaweza kutumia huduma ya One Network wakisafiri katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria, Niger, Chad, Malawi, Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Congo Brazzaville, Burkina Faso na Sudan. Mashariki ya Kati, huduma ya One Network inapatikana katika nchi za Jordan, Bahrain, Iraq na Saudi Arabia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain Group, Dkt. Saad Al Barrak alisema, “Tunaikaribisha Ghana katika familia ya Zain. Ghana ni muhimu kwa Zain na tumewekeza kwa nguvu zote ili kuleta teknolojia ya kisasa na huduma bora Magharibi mwa Afrika. Kutokana na mfumo wetu, tunawahakikishia watu wa Ghana watapata huduma bora ya mawasiliano duniani.”

Kutokana na Zain Ghana kujiunga katika huduma ya ‘One Network’, Bw. Chris Gabriel, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zain Afrika, aliongeza kwamba: “Kutokana na maelfu ya watu wa Ghana kuvuka mipaka kila siku kwenda Burkina Faso na katika nchi nyingine zenye huduma ya ‘One Network’ ya Zain kama Nigeria na Niger, huduma ya One Network itaendelea kupanuka wigo wake na kuwawezesha wapendanao kupata mawasiliano kwa urahisi, na kuboresha maisha kwa jamii.”

Wateja wote wa Zain barani Afrika na Mashariki ya Kati waliounganishwa katika huduma ya prepaid na postpaid, wanatumia One Network na hivi sasa wanaweza kusafiri kwenda nchi 17 wakitumia simu zao bila kutozwa bei zaidi ya ile ya kawaida na bila kulipia gharama ili kupokea simu zinazoingia.

Wateja wa Zain pia wanaweza kuingiza pesa kwenye simu zao wakiwa nchi hizo bila kununua kadi kutoka nchi anayotoka na zaidi ya vituo 150,000 barani Afrika na Mashariki ya Kati vinatoa huduma kwa wateja wa Zain popote walipo.

“Wateja wanaweza kupiga na kupokea simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa gharama za kawaida, kupokea bure simu zinazopigwa kutoka katika moja ya nchi 17 zilizounganishwa na huduma ya One Network. Huduma ya One Network kwa wateja wa prepaid inatolewa moja kwa moja katika nchi zote, na haihitaji mteja ajisajili wala kulipia ada," alisema Bw. Gabriel.

Zain inatambulika kwa kuongoza katika mageuzi ya teknolojia ya huduma ya mawasiliano ya kisasa kwa wateja inaowatumikia. Zain ilikuwa ya kwanza kuzindua huduma ya ‘One Network’ kwa zaidi ya watu milioni 100 nchini Kenya, Tanzania na Uganda mwaka 2006, na inaahidi kuendelea kutoa huduma bora za mawasiliano kwa wateja wa Zain

Zain yamwaga msosi kwa yatima Mtwara!!

Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Zain mkoani Mtwara wakiwa na baadhi ya watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Raha Leo EAG mjini Masasi, Mtwara mwishoni mwa wiki. Zain ilitoa bidhaa mbalimbali zenye thamani ya sh. 500,000 kwa kituo hicho.


Mratibu wa Maendeleo ya Biashara wa Zain Wilaya ya Masasi, Richard Kisse (mwenye fulana ya kijani) akikabidhi zawadi kwa Suzan wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Raha Leo EAG mjini Masasi, Mtwara mwishoni mwa wiki. Zain ilitoa bidhaa mbalimbali zenye thamani ya sh. 500,000 kwa kituo hicho.


Uzinduzi wa Tupendane ya JHIKOMAN umewadia!!

Show hii inayoletwa kwa hisani ya Goethe-institut Tanzania ( kituo cha utamaduni cha wajerumani). Ni uzinduzi rasmi wa Albamu mpya ya Jhikoman inayoitwa TUPENDANE.
Vilevile Wahapahapa Band wata tambulisha Albamu yao iitwayo BARUA itakayo zinduliwa mwakani.Ashimba jina jipya katika fani lenye mambo makubwa! Ashimba atatambulisha NURU NYIKANI Albamu itakayozinduliwa mwanzoni mwa mwaka 2009. Ashimba anafanya kazi chini ya Maisha Music.Wasanii wengine watakaoshiriki katika onyesho hili ni Vitalis Maembe, Misoji Nkwabi wote kutoka Bagamoyo. Antonia Kutoka Ujerumani. Sqeezer naye atakuwepo pamoja na wasanii wengine wengi!

USIKU WA KUJIACHIA NA NDOVU!!

usiku wa kujiachia na ndovumamboz!!hili ni onesho lililokusanya wanamuziki wa kizazi kipya nchini ambao ni Dully Sykes,Jay Moe,Mangwea,Mchizi Mox pamoja na Makamua na linatarajia kufanyika tarehe 24 mwezi huu ndani ya ukumbi wa ROYAL VILLAGE pale mkoani Dodoma.Zawadi mbalimbali zitatolewa kutoka kinywaji cha Ndovu Special Malt.Wakazi wa Dodoma ni zawadi maalumu kwao!wakae mkao wa kupokea vyuma hatari siku hiyo ya mkesha wa siku ya Chrismas.