Mabaharia wawazidi nguvu maharamia!!


Mabaharia waliotekwa na maharamia wa kisomali kwenye meli ya biashara inayomilikiwa na raia wa Libya wamefanikiwa kuidhibiti tena meli hiyo katika ghuba ya Aden.
Jeshi la majini la Ulaya linalopambana na uharamia katika pwani ya Somalia limesema baadhi ya maharamia wanaaminiwa kuuawa wakati wa tukio hilo.

Jeshi hilo la Umoja wa Ulaya, Navfor, limesema mmoja wa mabaharia katika meli ya biashara ya MV Rim amejeruhiwa.

Wakati huo huo, meli nyingine imetekwa katika ghuba ya Aden.
Maharamia wameteka meli hiyo yenye tani 15,000, MV QSM Dubai, katika ghuba ya Aden mapema Jumatano.

Meli hiyo ina mabaharia 24 yenye raia wa Ghana, Misri, Pakistan na Bangladesh.
Meli ya kivita ya Marekani imeripoti kuona angalau haramia mmoja kwenye meli hiyo iliyotekwa akiwa na guruneti.
'Taarifa za kukanganya'
Taarifa kutoka Navfor imesema, meli ya kivita ya EU, SPS Victoria, ilipelekwa kwenye ghuba ya Aden kutoa msaada wa kitabibu kwa mabaharia wa MV Rim.

Imesema kulikuwa na "taarifa za kukanganya" kwamba meli hiyo ilikuwa imevamiwa tena na maharamia.
Lakini helikopta kutoka meli hiyo ya kivita ilipofika kwenye eneo la tukio, iliweza kufahamika haraka kuwa mabaharia hao waliweza kudhibiti meli hiyo.

MV Rim, yenye mabaharia wake 10 kutoka Syria ilitekwa mwezi Februari na maharamia waliodai kikombozi cha dola za kimarekani milioni tatu ili kuwaachia wakiwa salama.

Baada ya kutekwa, waandishi wanasema maharamia waliivusha meli hiyo kwenye mji wa Laasgoray, mpakani mwa miji ya Somalia inayojitawala yenyewe ya Somaliland na Puntland.
Takwimu zilizotolewa na shirika la kimataifa linalosimamia safari za majini (IMB) zinaonyesha kuwa mashambulio ya maharamia duniani yameporomoka kwa asilimia 34 katika miezi mitatu ya mwaka 2010 ukilinganisha na mwaka mmoja uliopita, kutokana na kuwepo kwa meli za kigeni kwenye ghuba ya Aden.

Takriban meli 20,000 hupita kwenye ghuba ya Aden kila mwaka, zikielekea na kurudi kutoka mfereji wa Suez.

Wafanyakazi TBL washiriki kufanya usafi maadhimisho ya siku ya mazingira!!

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Richard Mfugale (kushoto), akimshukuru Ofisa Uhisiano wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Lillian Erasmus (kulia) ambaye alikabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi vyenye thamani ya sh.
milioni 2 kwa manispaa hiyo.Hfla hiyo ilifanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani eneo la Msimbazi
Bondeni, Kata ya Mchikichini, Dar es Salaam jana. Wafanyakazi wa TBL waliungana na wakazi wa eneo hilo kufanya usafi
wa mazingira. Katikati ni Renatus Nyanda ambaye ni Meneja Huduma wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa KIampuni ya Bia Tanzania (TBL), Nik Brooks (kushoto0 na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Robin Goetzsche (katikati) wakiungana na baadhi ya wafanyakazi wa TBL, kufanya usafi kwenye
mazingira yanayozunguka kiwanda chao, Jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya
Siku ya Mazingira Duniani.mtaro wa maji yatokayo kiwandani.



Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwa na baadhi ya wakazi wa eneo la Msimbazi Bondeni, Mchikichini,
Dar es Salaam, kufanya usafi katika eneo hilo ikiwa ni moja ya shamrashamra ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
jana.

MISS CHANG'OMBE KUONDOKA NA LAKI TANO IJUMAA!!

Meneja Masoko wa Kampuni Konyagi Nchini B.Martha Bangu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya Lamada wakati Mwandaaji wa Miss Chang'ombe Tom Chilala alipotangaza zawadi za washindi wa shindano hilo linalotarajiwa kufanyika juni 4 kwenye ukumbi wa TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam.
Katika shindano hilo linalotarajiwa kuwa la kuvutia kutokana na viwango vya warembo wanaoshiriki katika shindano hilo, burudani itatolewa na bendi maarufu jijini ya FM Academia wazee wa ngwasuma huku kundi la ngoma za asili la Machozi likinogesha burudani za shindano hilo ambalo ni la pili mara baada ya kumalizika kwa shindano la Miss Kurasini ambalo lilifanyika hivi hivui karibuni.
Akitangaza zawadi hizo Chilala amesema mshindi wa kwanza atapata shilingi laki tano, wa pili atapata shilingi laki tatu na wa tatu atapata shilingi laki mbili wakati wa nne na wa tano watapata shilingi laki moja kila mmoja huku kifuta jasho kikiwa ni shilingi elfu hamsini kwa kila mmoja.
Wengine waliopo katika picha katikati ni mratiobu wa Miss Chang'ombe Tom Chilala na mwisho ni Meneja wa kinywaji cha Redds Original Kabula Nshimo.
Mwandaaji wa Miss Chang'ombe Tom Chilala wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Kabula Nshimo Meneja wa bia ya Redds Original kulia, Martha Bangu Meneja Masoko wa Konyagi na mwalimu wa Warembo Vumilia Wilbroard pamoja na warembo wa Miss Chang'ombe.


WANAFUNZI WA CHUO KIKUU TUMAINI IRINGA WAKUTANA NA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI MAELEZO!!

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Clement Mshana akizungumza na wanachuo kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa hawapo pichani kwenye ukumbi wa Idara hiyo wakati wanafunzi hao walipotembelea idara hiyo leo kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na idara hiyo ambayo ni ya Serikali, wanafunzi hao wako jijini kwa ziara ya mafunzo ya uandishi wa habari na mambo mbalimbali yanayohusu taaluma ya habari kwa ujumla, ambapo wanatembelea vyombo mbalimbali vya habari katika picha kushoto ni Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya habari Maelezo Helman Hokororo na kulia ni Afisa habari mwandamizi wa idara hiyo Mwirabi Cisse .
Mwanafunzi wa chuo kikuucha Tumini Elsi Martin akifurahia jamabo katika mazuingumzao hayo yaliyowakutanisha na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Malelezo.
baadhi ya wanafunzi wakifuatilia mada iliyopkuwa ikitolewa na mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Clement Mshana
baadhi ya wanafunzi wakionekana kushauriana jambo.

JUNI 5-2010 NI MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA!!

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dr. Batilda Buriani akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya makamu wa Rais leo mchana wakati alipozungumzia siku ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, kulia ni Richard Muyungi Mkurugenzi msaidizi Mazingira.


Tarehe 5, Juni ya kila mwaka Watanzania tunaungana na mataifa mengine duniani kuazimisha siku ya mazingira duniani ambapo maadhimisho hayo kuwa ni sehemu ya kumbukumbu mambo mbalimbali ya mkutano wa kwanza wa umoja wa mataifa kuhusu mazingira uliofanyika mwaka 1972 mjini Stockholm Sweden.

Katika mkutano huo pia lilipitishwa azimio la kuunda shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia mazingira duniani (United Nations Enviromental Program) yani (UNEP).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa rais (Mazingira) Dk.Batilda Buriani amesema maendeleo endelevu ya nchi yetu yanategemea sana jinsi tunavyotunza mazingira yetu lakini zaidi ya asilimia 60 ya nchi yetu inakabiliwa na changamoto nyingi ya hali ya jangwa na ukame takribani hekta 220,000 za misitu hufyekwa kila mwaka kwa mahitaji ya nishati hususani mkaa,kilimo kilichoendelevu na biashara ya magogo,uwezo wa malisho katika mikoa mingi umezidiwa na wingi wa mifugo na hivyo kusabisha uharibifu mkubwa wa mazingira na uvamizi wa vyanzo vya maji.

Aidha Dk.Batilda amesema mazingira ya bahari yanaharibiwa kwa kiasi kikubwa hasa kutokana na Uvuvi usioendelevu na uchafuzi wa mazingira ya bahari kwa mfano takwimu zinaonyesha kushuka kwa samaki wanaovuliwa baharini kutoka tani 52,935 mwaka 2001 hadi tani 43,459 mwaka 2007 ambapo takwimu za kimataifa inakadiriwa kuwa miaka 40 ijayo uvuvi wa kibiashara unaweza usiwepo kabisa kutokana na uvuvi usio endelevu(over fishing).

Akihitimisha Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa rais Dk.Batilda Buriani ameziomba taasisi zote,mashirika yasiyo ya kiserikali na wananchi kwa ujumla kutumia fursa ya maadhimisho hayo kwa kushiriki katika shughuli za hifadhi ya mazingira katika maeneo yao na pia akiwataka waganga wa kienyeji ambao ndio watumiaji wakubwa wa misitu katika uchimbaji wa dawa na mabo mengine yanayohusiana na uganga wa kienyeji kulinda misitu.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya misitu kimataifa ni “VIUMBE NI WENGI.DUNIA NI MOJA NA MSTAKABALI MMOJA”Tunza mazingira kwa hifadhi endelevu ya viumbe hai,maadhimisho haya kitaifa mwaka huu kufanyika Mkoani Dodoma katika wilaya ya Bahi.

Miss Dar City Centre kuondoka na Milioni moja,Kusindikizwa na Machozi Band,Chege



Kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Dar City Centre 2010, kinatalajia kufanyika Juni 5 kwenye Hotel ya Moven pick jijini Dar es Salaam, huku mrembo wa kwanza wa shindano hilo akinyakua kiasi cha shilingi Milioni moja(1000000) na wapili laki saba(700000) na wa tatu akinyakua kiasi cha laki tano(500000)

Mbali na zawdi hizo kwa washindi hao, pia zawadi kwa mshindi waliobaki wataondoka na kifuta jasho cha shilingi 100000(laki moja moja0.

Katika shindano hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Millennium promoters, kundi la Machozi Band, sambamba na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ pamoja na Chege anayetamba na nyimbo ya ‘Mkono mmoja weka juu” watapagawisha mashabiki watajkaojitokeza kuangalia warembo hao.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Fortunatus Faustine, akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwatambulisha warembo hao mbele ya waandishi wa habari, ilipofanyika katika Ukumbi wa Savanna Lounge uliopo katika Hotel hiyo Paradise City Centre.(Posta Mpya).

Katika shindano hilo ambalo linatalajia kuanza majira ya jioni saa mbili usiku.Walitaja viingilio vya shindano hilo kuwa ni kiasi cha shilingi 25,000, kwa muda wa kawaida na getini itakuwa ni shilingi 30,000.mbali na hilo pia kwa upande wa VIP ambapo itakuwa pamoja na chakula cha usiku, ni shilingi 50,000.

Kwa Upande wake mratibu wa kituo hicho cha Dar City Centre, Cathelini John, alisema kuwa tiketi za shimndano hilo zimeanza kuuzwa katika sehemu za; Best Bite-Namanga, Savannah Lounge, Movenpick- Gift Shop, Chiken Hut-MIlimani City, Rose Garden -Pub, Best Bite -Namanga.

Pia Cathelini alisema kuwa warembo hao ammbao mpaka sasa wanajifua katika hotel ya Lamada chini ya aliyekuwa miss Tabata pia alishiriki shindano la Miss Tanzania, Flora Florence(22).

Aliwataka baadhi ya warembo hao kuwa ni pamoja na Glory Mosha (20), Agness Francice (20), Bahati Chande (20), Kiren Mohammed (20), Sara Nasoro (20), Suraina Merwiro (23), Neena Jackob (2o), Neema Alen (18), Mariam Hassan (19), Sara Said (20), Nance Mane (20) na Anabela Isaya(21).

MAADHIMISHO YA UHURU WA KENYA YAFANYIKA UWANJA WA NYAYO NAIROBI!!

Baadhi ya wananchi wa Kenya wakifurahia kupigwa picha wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
(Picha Zote na Anna Nkinda)

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga akiongea na waandishi wa habari wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Baadhi ya wananchi wa Kenya waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi wakigombania kupata nakala ya hotuba ya Rais Mwai Kibaki.

Baadhi ya wananchi wa Kenya wakifurahia kupigwa picha wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Wanafunzi wa shule ya Kaguma kutoka wilaya ya Tharaka, Mkoa wa Mashariki nchini Kenya wakicheza ngoma ya kabila la wameru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Askari Polisi wa kikosi cha mbwa wakitoa salamu za heshima kwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wakicheza gwaride la sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Askari wa kike kutoka Jeshi la Kenya wakitoa salamu za heshima kwa Rais Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wakicheza gwaride la sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Askari wa Bendi ya Jeshi la Kenya wakitoa salamu za heshima kwa Rais Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Askari wa Jeshi la Kujenga Vijana (National Youth Services) wakitoa salamu za heshima kwa Rais Mwai Kibaki (hayupo pichani) wakati wakicheza gwaride la sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya sikukuu ya madaraka ziliyofanyika jana katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Watu 18 wanyongwa Libya_AI


Shirika la Kutetea haki za kibinadam la Amnesty International limeilaani vikali uamuzi wa serikali ya Libya wa kuwanyonga watu 18 wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya kigeni.

Shirika hilo la Amnensty limenukuu habari kutoka kwa gazeti moja nchini Libya, linalomilikiwa na mwanawe kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muamar Gadaffi.

Ripoti hiyo iliripoti kuwa watu 18 wengi wao raia wa Misri na Nigeria, walinyongwa siku ya Jumapili, baada ya kupatikana na hatia ya kupanga mauaji.

Shirika hilo limesema limehuzunishwa na hukumu hiyo iliyotolewa nchini Libya baada ya kesi ambayo haitimiza masharti ya kimataifa kuhusu kusikilizwa kwa kesi kwa njia ya haki. www.bbcswahili.com

Wakenya watakiwa kuchangamkia soko la pamoja la Afrika mashariki!!


Na Anna Nkinda - Nairobi


Wakenya wametakiwa kuchangamkia mkataba wa soko la pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki ambao utawawezesha kufanya biashara, kazi na kuishi mahali popote wapendako ndani ya nchi wanachama, kupata fursa nzuri ya kuchuma mali zaidi na hivyo kujikwamua na maisha ya umaskini.


Wito huo umetolewa jana na Rais wa Nchi hiyo Mwai Kibaki wakati akiwahutubia wananchi kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya sherehe za sikukuu ya madaraka iliyofanyika katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Kibaki alisema kuwa mkataba huo ambao utasainiwa mwezi wa saba mwaka huu utatoa fursa nzuri ya kuchuma mali zaidi kwa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki, kubuni nafasi za kazi na kuondoa umaskini.

“Katika ngazi ya kanda hii , ni fursa yangu kuona kwamba mkataba wa soko la pamoja la Jumuia ya Afrika mashariki utaanza kutekelezwa hivi karibuni hivyo basi Serikali yangu inashirikiana kikamilifu na nchi wanachama wa jumuia hii kuhakikisha kuwa utendaji kazi wa vipengele vyote vya mkataba huu unakamilika”, alisema Kibaki.

Kibaki pia alitoa rai kwa wakenya kuwakaribisha kaka na dada zao kutoka nchi za Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda ambao nao wataingia katika nchi hiyo kujitafutia riziki na kusema kuwa hiyo ndio njia ya kuonyesha shukrani na moyo kwa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Aliendelea kusema kuwa hivi sasa wanapenda kufungua kabisa eneo la kaskazini Kenya na kustawisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji na majirani zao.

Serikali ya nchi hiyo hivi karibuni ilitoa kandarasi za kufanya uchunguzi wa ujenzi wa bandari ya Lamu, ujenzi wa reli kutoka Lamu kupitia Isiolo hadi Juba na kutoka Lamu-Isiolo hado Moyale.

Kibaki alisema “Ujenzi wa vifaa hivi vya muundombinu msingi utaanza hivi karibuni. Vilevile tumetoa zabuni ya kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Malaba na pia tutaimarisha zaidi huduma ya uchukuzi wa abiria kupitia magari ya moshi hapa jijini Nairobi”.

Kibaki alisema, “Matukia haya yakijumuishwa na uwekezaji tunaoufanya katika upanuzi wa barabara, utoaji wa nguvu za umeme, huduma za maji, huduma za simu na viwanja vya ndege ni ishara ya kutosha kwamba tunatayarisha nchi hii kwa hatua ya ubunifu wa nafasi za kazi na ustawi chini ya ruwaza ya maendeleo ifikapo mwaka 2030”.

Alifafanua kuwa ndiyo sababu hivi sasa wanaharakisha kazi za ujenzi wa barabara kuu ya Nauru - Eldoret hadi Malaba na kutoka Kericho hadi Kisumu na vile vile kupanua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kisumu ili kuhakikisha uchukuzi bora wa watu na ushiriki wa haraka wa masoko unafanyika.

Kuhusiana na uchumi wa nchi hiyo Mwaikibaki alisema kuwa mwaka jana uliimarika kwa asilimia 2.6 kutoka asilimia 1.6. Kwa mwaka huu unatarajiwa kukuwa zaidi kati ya asilimia 4 na 5 . Hii ni kwasababu wakenya hata wakati wa hali ngumu, wanaendelea kufanya kazi kwa bidii kuimarisha maslahi yao binafsi na ya nchi.


Naye waziri Mkuu wa Nchi hiyo Raila Odinga alisema kuwa wakenya kabla ya kupata uhuru walikuwa wananyanyaswa sana na mabepari wa kikoloni ambao walikataa kuwapa uhuru wao kwa madai kwamba hawawezi kujitawala.


“Hivi sasa tuko huru tunahitaji kuwa na katiba yetu wenyewe kwani katiba tunayoitumia sasa ilitungwa na wakoloni huko katika nyumba ya Lang’ata hakuna hata mkenya mmoja aliyeshiriki, baada ya miaka mingi tumeona ni vyema tuwe na katiba yetu wenyewe lakini bado kuna watu wanaopinga kama vile wakoloni walivyopinga kutupatia uhuru wetu”, alisema Odinga.

Aliwaomba wananchi waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya ndiyo tarehe nne Mwezi wa nane mwaka huu wakati wa kura ya maoni ili wakenya wapate katiba mpya waliyoiandaa wenyewe.

Kenya ilipata uhuru wake mwaka 1963 baada va mapigano yaliyosababisha watu wengi kupoteza maisha yao kutoka kwa wakoloni wa kiingereza.

Israel kuwaachilia wanaharakati!


Serikali ya Israel imeanza kuwaachilia wanaharakati waliokamatwa kwenye meli zilizokuwa zinapeleka msaada Gaza na kisha kuwarejesha makwao.

Kwa mujibu wa Israel, meli hizo zilishambuliwa baada ya kukiuka marufuku iliyowekwa na Israel kuingiza bidhaa zozote katika Ukanda wa Gaza.

Zaidi ya wanaharakati miamoja wa kiarabu wanatarajiwa kuachiliwa na kurejeshwa makwao, Israel ikilenga kukamilisha shughuli hiyo katika muda wa saa arobaini na nane.

Takriban wanaharakati tisa wa kipalestina walifariki wakati makomandoo wa Irsrael waliposhambulia meli sita zilizokuwa zinaelekea Gaza siku ya jumatatu zikiwa zimebeaba msaada wa chakula na bidhaa zinginezo.

Hata hivyo Israel imetetea hatua ya wanajeshi wake ikisema walikuwa wanajilinda kutokana na uvamizi wa wanaharakati hao, ingawa wanaharakati wenyewe wamekanusha madai hayo. www.bbcswahili.com

WANANCHI 300 WAVAMIA KITUO CHA POLISI HEDARU NA KUCHOMA MOTO!!

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema akizungumza na waandishi wa habari mchana huu kwenye makao makuu ya jeshi hilo wakati alipozungumzia uvamizi wa kituo cha polisi cha Hedaru uliofanywa na wananchi 300 baada ya kuvamia kituo cha polisi na kuchoma moto pamoja na magari matatu na nyaraka mbalimbali kituoni hapo.
Akifafanua zaidi IGP Said Mwema amesema mnamo tarehe 28-5-2010 mtoto mdogo aitwaye Garce Garce Kelvin mwenye umri wa miaka 5alitoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha akiwa anatokea shule ya chekechea katika mji mdogo wa Hedaru, baadae katika hatua za ufuatiliaji zilipokelewa taarifa kuwa mtot huyo amepelekwa katika kijiji cha Chome Mlimani katika msitu wa Shengena ambako pia kuna machimbo ya Dhahabu kwa imani za kwamba huenda ameenda kutolewa kafara huko kwa imani za kishirikina.
Tarehe 30-5-2010 mkuu wa kituo akiongozana na wapelelezi walifuatilia taarifa hizo zilizopokelewa kutoka kwa wananchi ambapo katika oparesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wapatao sita na waliendelea kuhojiwa katika kituo cha polisi Same.
Mnamo tarehe 31-5-2010 kulitokea kundi lingine la vijana waliokwenda katika msitu wa Shengena kijiji cha Chome ikidaiwa walipata taarifa kwamba mtoto huyo amepelekwa kutolewa kafara kwenye machimbo ya dhahabu kwa imani za kishirikina, hata hivyo vijana hawa hawakufanikiwa kumpata mtoto badala yake waliwakamata watu nane wanaume saba na mwanamke mmoja waliowakuta na vifaa vya uchimbaji wa madiniya dhahabu na kuwapeleka kituo cha polisi Hedaru.
Majira ya saa mbili usiku tarehe hiyohiyo watuhumiwa wakiw akituoni Hedaru uvumi ulizagaa kwamba watu waliokamatwa na kundi la vijana ndiyo waliohusika na kutoweka kwa Grace Kaelvin hivyo kundi la wananchi 300 walivamia ktuo cha polisi na kuchoma moto kwa nia ya kutaka kuwauwa watuhumiwa hao, hata hivyo hakuna vifo vilivyotokea baada ya polisi kufanikisha kuwatorosha watu hao , leo tarehe 162010 mtoto Grace aliyetoweka aliokotwa sokoni eneo la Pasua na kwasasa anapelekwa kuungana na familia yake zaidi yahapo watuhumiwa watano wamekamatwa kwa kuchoma kituo.
Mwema amesema tabia ya kushambulia vituo vya polisi kwa hisia au kuchukua sheria mkononi kunavuruga amani na utulivu nchini, lakini pia ni uvunjaji wa sheria
IGP Said Mwema akizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo leo mchana huku akiwa na mamakanda wa vitengo mbalimbali kutoka kushoto ni ACP Abdallah Mssika, ACP Hassan Mbezi, ACP Felix Mboya, ACP Hezron Kigondo na ACP Rashid Seif.

Rais Kikwete na Rais Museveni wahudhuria Misa ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere nchini Uganda!!

  1. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiagana na Mama Maria Nyerere muda mfupi baada ya kumalizika kwa misa Maalumu ya Kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili atangazwe kuwa Mwenye Heri iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mashahidi wa Uganda huko Namugongo, nje kidogo ya mji wa Kampala leo asubuhi.Misa hiyo iliyohudhuriwa pia na baadhi ya waumini kutoka Tanzania ni sehemu ya mchakato ilioanzishwa na kanisa Katoliki Tanzania wenye nia ya kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa Mwenyeheri na hatimaye Mtakatifu kulingana na vigezo na kanuni zilizowekwa na Kanisa hilo.
    Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya ibada maalumu kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa la Mashahidi wafia dini wa Uganda huko eneo la Namugongo, nje kidogo ya jiji la Kampala leo asubuhi.Wa kwanza kushoto ni Askofu Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba na wapili kushoto ni Dr.Cyprian Lwanga Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Kanisa Katoliki Kampala.



    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiasalimiana na baadhi ya Watanzania waliohudhuria ibada maalumu ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kanisa Katoliki ya Mashahidi wafia dini wa Uganda huko eneo la Namugongo, nje kidogo ya jiji la Kampala(picha na Freddy Maro)



JAMAL MALINZI ATOA MAPENDEKEZO YAKE KATIKA RASIMU YA KATIBA YANGA

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga Jamal Malinzi akiongea na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa mapendekezo yake juu ya marekebisho ya rasimu ya katiba ya Yanga kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa timu hiyo uanaotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Dare es salaam kwenye ukumbi wa Police Officers Mess.
Jamal Malinzi ametoa moja ya mapenddekezo yake kuwa Yanga wanatakiwa kuwa na kamati yao ya rufaa itakayomaliza matatizo yao hapohapo klabuni badala ya mtu kutoka nje kuwachagulia viongozi kama ilivyotokea kwa timu ya Simba hivi karibuni ambapo kamati ya uchaguzi ya Simba ilimpitisha Zakaria Hanspope kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo lakini kamati ya Rufaa ya TFF ikamkata jina lake.
Hata hivy Simba wamemchagua tena Zakaria Hanspope kwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu hiyo lakini sijasikia TFF wakitoa tamko lolote juu ya hilo kwa hiyo hiyo ndiyo picha ninayoiona na ndiyo mambo ambayo sitaki yatokee ndani ya Yanga, Lakini wanachama wa Yanga wanayo haki ya kuyakubali mapendekezo yangu au kuyakataa huo ni uamuzi wao.

Israel kuchunguzwa na Umoja wa Mataifa!!


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kuanzishwa uchunguzi huru kufuatia shambulio kwenye meli za kibinadamu zilizokuwa njiani kupeleka misaada katika ukanda wa Gaza.

Taarifa ya Baraza la Umoja wa Mataifa imetokea baada ya mashauriano yaliyochukua usiku kucha. Takriban wanaharakati 10 waliuawa wakati wanajeshi wa Israel walipoingia ndani ya meli hizo kwenye mipaka ya kimataifa.

Taarifa hiyo imeafikiwa kati ya Uturuki na Marekani, huku Uturuki ikisisitiza laana kali dhidi ya Israel nayo Marekani ikaamua kutotoa maneno makali kwa mshirika wake huyo wa karibu.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani matukio yote yaliyosababisha vifo vya watu 10 na wengine wengi kujeruhiwa pamoja na kufariji familia za waathirika.

Aidha baraza hilo limetaka meli hizo ambazo zinazuiliwa mwambao wa Israel kuachiliwa mara moja. Punde baada ya taarifa hizo kutolewa wapiganaji kadhaa wa Kipalestina walivuka mpaka na kuingia upande wa Israel ambapo walikabiliana na wanajeshi huku wawili wakiuawa.

Kwa upande wake mwakilishi wa Israel katika Umoja wa Mataifa amesema wanajeshi wake walikuwa wakijikinga kutoka mashambulio ya wanaharakati hao.

JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI YAIAMINI VODACOM TZ!!

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji cha Taifa Emmanuel Ole Naiko (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Dietlof Mare cheti cha kuaminiwa kutoka Jumwiya ya Afrika Mashariki, Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwake, (Mpiga picha wetu)

Ndovu Special Mart Ilivyonyakua tuzo yake!!

Meneja wa Ndovu Oscar Shelukindo na mpishi mkuu wa TBL Mzee Gaudence Mkolwe wanatarajiwa kupokewa kwa shangwe watapotua Dar Jumatano Mchana na Gulf Air wakitokea nchini Ujerumani walikokwenda kupokea tuzo ya Monde Selection baada ya bia ya Ndovu Special Malt kushinda tuzo hiyo na kuwa bia bora duniani.
Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt Oscar Shelukindo akiwa ameshika cheti cha ushindi huo.

Furaha na fahari ya Grand Gold Award ya Ndovu Special Malt

Mmoja wa Watanzania waishio Ujerumani akijiunga kushangilia ushindi wa Ndovu.

Ndovu Special Malt ikitangazwa mshindi wa tuzo ya Grand Gold
Oscar Shelukindo na Mzee Gaudence Mkolwe wakipokea Grand Gold Award ya Ndovu Special Malt jijini Wiesbaden, Ujerumani, usiku kuamkia leo.