MTOTO WA WAZIRI MKUU AIBUKA KIDEDEA UVCCM UBUNGE!!

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Mtoto wa tatu wa Waziri Mkuu Mizengo Peter Kayanza Pinda Bi.Fotnata Kayanza Peter Mizengo Pinda (26) ameibuka kidedea baada ya kuwa miongoni mwa vijana 10 wa UVCCM saba wakitoka Bara na watatu Visiwani Zanzibar watakaowakilisha wenzao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitokea mkoa mpya wa Katavi baada ya mkoa wa Rukwa kugawanywa mara mbili.




Bi. Fotnata Pinda ambaye ni mtumishi wa Serikali akiwa ofisa katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma amechaguliwa katika mkutano wa Makamanda wa Vijana wa UVCCM uliofanyika huko Dodoma siku ya jana na kumalizika leo asubuhi.




Bi. Fotnata Pinda anaonekana kufuata nyayo za baba yake Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Mtoto wa Mkulima)ambaye amekuwa mtetezi wa watu kwa vitendo na amekuwa mahiri katika kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kujenga hoja zenye usawa mara nyingi wakati anapojibu maswali ya ana kwa ana kutoka kwa wabunge Bungeni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment