Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mhe. Celina Kom bani (kushoto)na wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi ndugu Betty Mkwasa wakimsikiliza Ofisa mwandamizi wa Karadha ya Fedha ,Benki ya Rasilimali Tanzania ni ndugu Betty Massanja kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma, Maonesho hayo yanatarajiwa kumalizika tarehe 8 Agosti mwaka huu.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mhe. Celina Kombani wa pili kulia akimsikiliza kwa makini Ofisa wa Kilimo (Kilimo na Lishe) ndugu Stella Kimambo jinsi mashine iliyopo mbele yao ijulikanayo kama (Cassava Grater)inayosaga Mhogo mbichi na kupata machicha ambayo unaanika nakusaga tayari kwa unga au unaukamua tayari kuwa wanga na ukautmia kama dawa ,na pia ukatumika kwa kutengenezea chapati ,kwenye maonyesho ya nanenane Mkoani Dodoma. (Picha zote na Anna Itenda- Maelezo).
Mwenyekiti wa kikundi cha Tupendane kilichoko katika kijiji cha Nala Wilayani Dodoma Bwana Peter Lenjole akimpa maelezo jinsi wanavyotumia Trekta ndogo za kulimia (Power Tiller) Waziri wa nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)Mhe.Celina Kombani (wanne kushoto) kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma
0 comments:
Post a Comment