MSONDO KUTOA BURUDANI MBAGALA ZAKHEM!!


BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma inatarajia kutoa burudani katika sherehe za mbio za mwenge zitakazofanyika jumapili Mbagala Zakiem, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema, kutokana na kushiriki katika maadhimisho hayo hivyo bendi hiyo haitaweza kutoa burudan katika onesho lao la kila jumapili linalofanyika katika Ukumbi wa Africenter, Ilala jijini Dar es salaam.

Alisema, kutokana na sababu hizo uongozi wa bendi hiyo unawaomba radhi wapenzi wa bendi hiyo kwa usumbufu utakaojitokeza ambapo wataendelea na burudan hiyo kwa jumapili ya wiki itayofuata.

"Tunawaomba radhi mashabiki wetu kutokana na hali hiyo kwa hiyo ni moja ya utendaji na majukumu ya bendi hiyo katika kutoa burudan katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na shughuli za kiserikali hivyo wataungana nao katika jumapili ya wiki itaakayofuata," alisema Super D.

Super D amewatakia wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake kuhudhuria kushuhudia burudani hiyo watakayoitoa nyimbo zao mpya ambazo ni miongoni mwa nyimbo zitakazo kuwa katika albamu yao mpya ya mwaka huu ikiwa ni pamoja kusikiliza nyimbo zao za zamani.
Alizitaja nyimbo hizo mpya kuwa ni Mjomba, Dawa ya deni kulipa na lipi jema ambapo albamu hiyo inatarajia kuachiwa mwishoni mwa mwaka huu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment