MASHUJAA MUSICA KUWASHA MOTO MANGO ALHAMISI 29 JULY 2010!!


Bendi ya Muziki wa Dansi inayokuja kwa kasi hapa nchini Mashujaa Musica siku ya Alhamisi kwa mara ya kwanza itafanya onyesho katika ukumbi wa Mango Garden kuanzia saa mbili usiku.



Akizungumza na vyombo vya habari Msemaji wa Bendi ya Mashujaa Shaaban Mpalule alisema kuwa burudani hiyo imeandaliwa maalumu kwa lengo la kuitambulisha bendi hiyo kwa mashabiki wa eneo la kinondoni ‘ Kama unavyofahamu tena ndugu yangu, bendi yetu ndiyo kwanza iko mbioni kujulikana ila nashukuru kwamba watanzania wameanza kuiona na tayari imeshapata mwelekeo mzuri kitu kinachotupa imani ya kufanya vizuri wakati ujao.



Kikubwa tunawaomba mashabiki wetu na wengine wote wajitokeze kuiunga mkono bendi yetu hii, na pengine niseme kuwa onyesho la Mango kwa kuwa litakuwa la kwanza kwa Mashujaa kutumbuiza katika ukumbi huo, mashabiki watakaokuwa wa kwanza kufika watapata ofa ya kuingia bure, isipokuwa tunawakaribisha wote wapenda burudani’ alisema Mpalule Aidha onyesho hilo litasimamiwa na Kiongozi Mkuu wa bendi hiyo Edward Malikidogo(Jadol Fidifosi FFU), sambamba na mkali wa kurapu Ibrahim Milinda Nyeusi(Vuvuzela), pamoja na mtaalamu wa Masauti Pasia Budansi.



Nyimbo zinazotarajiwa kuimbwa siku hiyo ni pamoja na nyimbo zao zote ikiwemo Moshi wa Sigara Mtunzi Pasia Budansi, Mwanike uliotungwa na kundi zima la Mashujaa, Safari ya vikwazo uliotungwa na Jadol FFU, Deodattha uliotungwa na Amosi Nabii Profiti, (Baba Mwenye nyumba asiyeogopa wingi wa siafu), Mama mi nashangaa uliotungwa na Ibrahim Milinda Nyeusi(Vuvuzela) Kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa ni cha chini ili kuwawezesha wote kuingia kupata burudani hiyo ambayo imepangwa kuwa shilingi elfu tatu kwa mtu mmoja na tiketi zote zitapatikana mlangoni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment