Jamani CRDB liangalieni upya hili magari mmetoa yasaidie wanafunzi kutokana na adha wanayoipata kwenye madaladala, lakini hao UDA mliowakabidhi jukumu la kusimamia mradi huo tayari wameshaanza kugeuza magari hayo na kuyafanya ya mradi wao wa kusanya abiria.
Kama inavyoonekana katika picha hii abiria wanapitia hata madirishani ili kuwahi viti wakati wanafunzi wanaonekana wakishangaa pengine ni kutokana na kitendo hicho cha wafanyakazi wa UDA kutotekeleza wajibu wao waliokabidhiwa na Benki ya CRDB kikamilifu katika kuendsha mradi huo wa mabasi ya wanafunzi na kuugeuza mradi wao binafsi wa kijipatia kipato, hii inatia aibu jirekebisheni.
Hizi ni dalili za wazi kabisa kwamba bado wanafunzi wataendelea kupata shinda hata kama magari haya yatapita mbele yao hebu watendaji wa UDA oneni aibu basi muachane na vitendo hivi vya kutia aibu. picha kwa hisani ya (Mo blog)
MABASI YALIYOTOLEWA NA CRDB BANK KWA WANAFUNZI YAGEUZWA MRADI WA WAFANYAKAZI WA UDA!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment