Bronislaw Komorowski na mkewe Anna.
Bronislaw Komorowski, ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanywa siku ya Jumapili nchini Poland.
Kwa mujibu wa televisheni ya taifa TVP, Komorowski amejikingia asilimia 53 ya kura zilizopigwa wakati mpinzani wake, Jaroslaw Kaczynski amepata asilimia 47.
Kaczynski ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kinachofuata sera za mrengo wa kulia, "Law and Justice" na ni ndugu pacha wa rais Lech Kaczynski alieuawa katika ajali ya ndege mwezi wa Aprili.Uchaguzi wa rais umeitishwa kufuatia kifo hicho.
Matokeo ya uchaguzi huo humaanisha kuwa Komorowski wa chama cha kiliberali cha "Civic Platform" na mshirika wake wa karibu, Waziri Mkuu Donald Tusk wataweza kuidhinisha marekebisho ya kifedha kabla ya uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanywa mwakani .

(24 SEVEN BLOG)
0 comments:
Post a Comment