![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwInJcu5pCGxTV-1iVJPGBDyoARhD7OZdFcs00CFmVkvxjTBbvuKBVPfriu43WVvItd4rtFQdDrFyFvxMN-vS-4zbqtwqZKZIf5HX1h5ahDtFPsC81cw7_CzmBL7jrBx_H5sZj4wyzXgmt/s400/IMG_4650.jpg)
M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 11 (Thursday July 29, 2010)
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwInJcu5pCGxTV-1iVJPGBDyoARhD7OZdFcs00CFmVkvxjTBbvuKBVPfriu43WVvItd4rtFQdDrFyFvxMN-vS-4zbqtwqZKZIf5HX1h5ahDtFPsC81cw7_CzmBL7jrBx_H5sZj4wyzXgmt/s400/IMG_4650.jpg)
0
comments
Saturday, July 31, 2010
FIESTA JIPANGUSE 2010 ILIVYOFANA MJINI MUSOMA !!
Posted by
ADMIN
Rais karume alipopiga kura ya maoni zanzibar jana!!
Posted by
ADMIN
Karume,akitumbukiza kura yake,katika kituo cha kupigia kura ya Maoni, ya kuwezesha Uundwaji Serikali ya Kitaifa ya Zanzibar,katika Skuli ya Msingi ya Kiembesamaki Wilaya Magharibi jana,Uundwaji wa Serikali hiyo ya Kitaifa ni baada ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Octoba mwaka 2010.
MABALOZI WA MALARIA WATOA MSAADA WA VYANDARUA KWA WAJAWAZITO MWANZA!!
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgstlsJkzeoQeE_oiH3-PTX-xzwtDzCa4r14dtE5wnKrjEssAcF0QR7V3wQbFxW0aP0mGJvzvO9ea28qxfIOvoILmgkjvFLvuC8qRzE-BSZNSeC0Hz-kPkLh7t_4JxfZJ3ZIB9LOQxq-a_w/s400/6.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjK9N3P-RdlVf6Kp_QgdqjgAb55IPfUL-CZF3eoX3Z7eXM5eilhL-wsfb14Cz0QI0y8Fk4SNsUUILTmL3dxhz27mW-QadEQvH6TNH3bOzikcYCCHr39VeMOxV5iZaY5JtdgH73ndDgDE_u/s400/8.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrhvUKeeLyjLLJXmplS0ygqfDf21XrGEnVHHUJEOn8oj-GoF4EG9g-cb2b_766MzDucI2haGZusmsEMCQs4i928DSC3jPVeNl-2usng34MOQjgIM_n8yoqYOUdZd5PyJUpPnp5FJlUgOFj/s400/4.jpg)
BASI LA NAJMUNISA LAPATA AJALI NA KUSABABISHA VIFO KADHAA!!
Posted by
ADMIN
Katika ajali hiyo inasemekana askari aliyekuwa akisindikiza basi hilo alikatwa kicha baada ya fuso kuharibiwa vibaya na basi. hebu Jionee mwenyewe picha zilizopigwa katikaajali eneo la tukio huko Kanegele kama inavyoonekana Sura ya Basi la Super Najimunisa baada ya Ajali.(Picha na Bernard Kinte wa mtandao wa Wanabidii)
HAKIKA UKIONA FILAMU HII HUTOAMINI KAMA NI MIMI NIMECHEZA..... NI CRAZY LOVE (KANUMBA)
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj63BLKdatpzF4fa4Oh8jW90TdJUE2LYSQndFbkd2dDoaZNhsJC-vf13DKbIVtV89sxtwPHRbijiQGSYPziGKVyQ7dTa7NngmPurXIV9CYIyIsvU7SHj2YNSXcIGRRrBIyy0hYnCBkhIndG/s400/cr2.jpg)
TAFADHALI FILAMU HII SI YA KUKOSA,PATA NAKALA YAKO ORIGINO,, FILAMU HII IKITOKA NAOMBA MNIAMBIE KWA KUNITUMIA E MAIL MBALI ILI KUNIPA MAONI KAMA MUIGIZAJI WA BONGO AMBAYE NIMEWEZA KUCHEZA UHUSIKA HUO?NINA UHAKIKA MAONI YENU YATAKUWA CHANGAMOTO KWANGU KATIKA KUCHEZA FILAMU NYINGINE NGUMU NA NZURI ZAIDI YA HII.
Hapa akionekana katika taswira nyingine ya Crazy Love.
Hapa Steven Kanumba akijipa raha huko Zanzibar hivi karibuni.
Hapa ni kivazi cha jioni, akiwa amejipigilia suruali yake ya kiaina fulani kama wenzetu kutoka kule bara la Asia.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiwG8vTFAsWuwsybQj2vxqB4ZxVw9Wzf1v8HaFvBa32oYxjRwHock2ls3derPW38GT8hYxmZGjP9WrB__qTc9VTb8j8vwCzqC7oggX3ovO-Bif9b4byMGL6paXVGaj-YK2gCI0XN47Mp69A/s400/cr1.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLAkyaKfKbRDceoVAQJtA7AwJQ1vhSHa3Za9mtgHKUQzFUl5G8MO9-mIyAAZ794KQv042vbGDbn3ursQsjWggpHa9YPpPrronQBF6SrcJplMZbVK1ApcDMhYH0jjyK5-dhhxsK7-M0W6fb/s400/kdm2.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyx5yZlJEAS_63XFGoU9TJD5bEbJ5D-9tKdIzgrfXfjXrKVnoA-w0N_CxqlI1jtl9ZLVi0x2LK8zUu5emmqtY87bxCHK4-l2CdGuMTbMb-1wBm70GACjtqdYJISuhTfJN3eh0JBoo6Hmnh/s400/kdm1.jpg)
0
comments
Friday, July 30, 2010
TIMU YA TAIFA YA MISRI KUIPA SOMO TAIFA STARS!!
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYhhN2ws9H4gx0-fccSRwqG4GviBlQU2KxrvQXHka5-W8Gi3PVOtU-TokQDItLARZhT2FZN2uy7reL_YkTbrQeRIdObHBkoN93xZT1NbKQ3Y4bYYn7ZTXcrfrRbU5G49r4M2cpT_1cmIsB/s400/TAIFA_STARS_CHAN_SQUAD%5B1%5D.jpg)
Msemaji wa TFF FLORIAN KAIJAGE amesema katika harakati za kutafuta timu wamefanikiwa kupata timu ya Misri.
Mchezo huo unatambulika na FIFA kwani siku hiyo ya mchezo ni siku iliyopangwa na FIFA kwa ajili ya mechi za kirafiki za FIFA.
Wakati stars ikijiandaa na mchezo huo tayari kocha wa timu ya stars JAN PAULSEN anatarajia kuwasili jumamosi usiku kuja kukinoa kikosi cha Taifa Stars. Habari na
M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 11 (Thursday July 29, 2010)
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMDWKbbfM6bkKlUlSHH5Qb37H0H_NvLar0Vx3PBFwDda_sh4qXxsm4FTGCY3ayyctETbSbTnRP1cp7oT_Az0s162-6axOmH2suhRatY0KV0bhyphenhyphenH9SFeQApRU0Aq8k6wFsqBfDEbxfs9Rm6/s400/IMG_4415.jpg)
M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 11 (Thursday July 29, 2010)
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEho4lRj6y_wSqoATlvTJ1PNdM-qR2dYyS9bVdOl7gc4Qm1ccibe04qfDu4lroCp4SK4Z7GYvbgv-hsPN8Rd21_rvtUUHBXockThpwpOvwtlKU46ZV38fet37Ujrwi3_z3ZJUUhyJF0c9Kgd/s400/OH.jpg)
RAIS JAKAYA NA ASKOFU WA KKKT MOROGORO NA WAZEE WALIOPIGANA VITA MKUU YA PILI YA DUNIA!!
Posted by
ADMIN
CD "Jakaya Kikwete 2010" kutoka kwao "Ngoma Africa Band" yatua nchini!!
Posted by
ADMIN
Hayawi !Hayawi ! Sasa yamekuwa ile CD inayozungumziwa na washabiki wengi kila kona duniani Sasa imeshatua nchini .
CD hiyo yenye jina "JAKAYA KIKWETE 2010" Kutoka kwao "The Ngoma Africa Band" bendi yenye maskani yake huko Ujerumani, Sasa unaweza kupata kopi za CD hiyo kwa ANKAL Muhidin Issa Michuzi aka Mzee wa Libeneke, kwa simu 0754271266 wa blogu ya jamii.
Pia kwa yeyote yule anayetaka atumiwe mp 3 au kuweka nyimbo hizo katika mlio wa Simu za viganjani tafadhali usisite kuwasiliana na Ankal Michuzi kwa simu namba 0754271266 CD hiyo yenye muziki mtamu unaosindikiza ujumbe muhimu kwa watanzania zaidi ya milioni 40.
Hivi sasa CD hiyo ipo nchini na unaweza kupata kopi yake na kuitumia katika sherehe ,mitaani,katika biashara yako,ndani ya mabasi,harusini,sokoni n.k, ili upate raha na ujumbe uliomo katika CD "Jakaya Kikwete 2010" utunzi wake Ebrahim Makunja a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU wa Ngoma Africa Band.
Pia Jumamosi ya 31-07-2010 saa 4 asubui Ras Makunja atahojiwa na radio Free Africa ya Mwanza tafadhali tega sikio.
Emirates Cup live on SuperSport
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjA_4OVe9Dlc-4F6z2lWyI0Cg-P89ChQjhOe8tko3baIH1oyXdMj-GT2PsXrgfSInU0ld2ueZuqBMYz17YV39aK6qm192cQqqRt1kbV_qeODfDgplXrka4Vyxq6m2Mqu9XrMOEr0UgOOPrD/s400/image001.jpg)
MWAKA HUU VIJANA WAMEVAMIA BUNGENI, NI KAZI KWELI KWELI!!
Posted by
ADMIN
Na Hillary Shoo,Singida.
KATIBU wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya (UNA) United Nation Asociation iliyopo kwenye jengo la umoja wa mataifa jijini Dare s salaam Fancy Nkuhi (25) amechaguliwa kuwa mmoja wa wagombe Ubunge kundi la vijana kutoka mkoani Singida.
Fancy aliibuka kidedea kwa kupata kura 16 kati ya kura 29 zilizopigwa jana na wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoani hapa.Katika uchaguzi huo mshindi alipata upinzani mkali kutoka kwa msindi wa pili Jamila Hasan aliyepata kura 10 huku Vailet Eliasi ambaye ni mfanyakazi wa ofisi ya UVCCM makao makuu akiambulia kura 3.
Mjasiriamali kutoka Kinondoni Mosi Ntandu aliambulia patupu baada ya kupata kura sifuri.Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo Fancy mwenye shahada ya sheria kutoka chuo kikuu huria,alisema matarajio yake ni kuhakikisha fursa wanazopata vijana katika nyanja mbalimbali zinafanikiwa.
Alisema atahakikisha kuwa fursa hizo zinapata msimamizi mwenye uwezo wa kuzitetea katika bunge pindi atakapochaguliwa kushika nafasi hiyo.Hata hivyo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Pascal Mabiti aliwataka vijana hao kuunganisha nguvu ya pamoja na kuvunja makundi ili kuhakikisha mwakilishi huyo kutoka mkoani hapa anaibuka mshindi katika awamu ya pili Mkoani dodoma Agosti 3 mwaka huu.
The French Government has provide 14 scholarship to Tanzanian!
Posted by
ADMIN
Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam
The French Government has provide 14 scholarship to various Tanzanian teachers to undergo in France a one month course on French language and training programme of French as a Foreign language.
The scholarship under a French project on Assistance in teaching of French in Tanzania has been allotted to teachers from Secondary School, University of Dar es Salaam and from the college o Business Education.
According to the French Embassy Communication Officer Joseph Kithama, other educationists to have been awarded a scholarship are inspectors of Primary and Secondary School and Curriculum planes from Tanzania Institute of Education (TEI).
Since 2008, Ministry of Education and Vocational Training in collaboration with the French Government is implementing a comprehensive action plan to enhance the teaching and learning of French in Tanzania. The French government is committed to assist education and wasters sectors in Tanzania through specific interventions agreed under a bilateral agreement between the two countries. French Ambassador to Tanzania Hon.
Jacques Champagne de Labriolle is scheduled to host a brief reception on July 30th, 2010 to departing Tanzanian educationist.”Bon Voyage”. In November 2009, a batch of 23 Tanzanians teachers went to France for a similar course, aimed at improving their level of French and their capacity to teach the language.
TAMASHA LA SAUTI YA KISWAHILI KURINDIMA JIJINI AGOSTI 4-6!!
Posted by
ADMIN
Katika tamasha hilo kutatolewa tuzo ya Mama Salma Kikwete kwa washindi ambapo pia mke huyo wa rais Atakuwa Mgeni rasmi ili kufanikisha tamasha hilo, katika picha kushoto ni Yusta Daniel Nyakachala Mkurugenzi wa Art In Tanzania na kulia ni Halima Kinungu Mhadhiri Chuo Kikuu Huria kitivo cha Sayansi na Jamii
HAYA NDIYO MAMBO YA DR. WILBROD SLAA LEO JIONI JIJINI ARUSHA!!
Posted by
ADMIN
2
comments
Thursday, July 29, 2010
SIMBA YAMNASA TENA KOCHA MSERBIA MILOVAN CURKORVIC!!
Posted by
ADMIN
Timu ya Simba leo imetangaza kuingia mkataba mpya wa miaka miwili na kocha Mserbia Milovan Curkovic ambaye atawasili wakati wowote kuanzia sasa ili kuja kuinoa timu hiyo, awali kocha huyo aliwahi kuja nchini na kufundisha timu ya Simba kabla ya kurudi kwao Serbia kutokana na kutoelewana katika baadhi ya vipengele kwenye mkataba wake wa awali
Simba imetangaza azma hiyo baada ya kusumbuliwa mara kwa mara na kocha wao Mzambia Patrick Phiri ambaye amekuwa msumbufu kwa muda mrefu mara inapotokea anakwenda lilikizo kwao Zambia, hivyo vitendo vya kocha huyo kupelekea kuwachosha wanasimba, jambo lililofanya uongozi kufikia uamuzi wa kutafuta kocha mwingine.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi Afisa Utawala na Kaimu Katibu mkuu wa klabu hiyo Evodias Mtawala, amesema hata hivyo kabla ya yote wamemtumia barua ya kumtaka kujiuzuru Kocha Patrick Phiri kutokana na kukiuka makubaliano na klabu hiyo hivyo kuifanya klabu hiyo kuhangaika katika suala zima la mwalimu.
Wakati huohuo Mtawala amesema Simba inatarajia kufanya tamasha lake la Simba Day Agosti 8 mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru ambapo timu za Express ya Uganda zimealikwa pamoja na timu ya Azam FC ya jijini, wakati Express ikicheza na Simba siku hiyo Azam itacheza na Simba B katika mchezo mwingine katika kufanikisha tamasha hilo.
ASHA ROSE MIGIRO ATEMBELEA TUME YA HAKI ZA BINADAMU.
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg6eCcb06c38IIACkYzAX2NMof36vhPDZRi6xR8YRpIEMH203dLTVwVLeMQmfPLQljTSadbDvSIa8E95OpsLgoH7_JDBTGukv1d6FTF4K9iV5uyb4ThBr_bZg0HP9Fb90DyLedcPC8XnPjK/s400/IMG_6654.jpg)
(PICHA NA ANNA ITENDA -MAELEZO)
M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 9 (Tuesday July 27, 2010)
Posted by
ADMIN
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgABTCXnf3UWR-LohsflMnhanVc4sMi8NxmS3_9T7Zd7XneZRyrLEXpxSA9FN4Bc_9aZGAHKTr-icuPjHJwbP1u9yHYWEy-7FkjAV0-nLDAHPzWn-xZVSaNvyrp1A-767Ww_t45mnK0ex6j/s400/IMG_4293.jpg)
Kapumzike kwa amani mpiganaji mwenzetu Primtiva Pancars.!
Posted by
ADMIN
Marehemu Primtiva alifariki juzi mkatika Hospitali ya Lugalo baada ya kuugua ghafla na kupoteza uhai wake,Marehemu atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuandika habari na makala zenye mguso kwa jamii hivyo kujipatia heshima kubwa kwa wasomaji wake ingawa alikuwa bado mchanga kwa kiasi fulani katika fani hii ya uandishi.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Primtiva Pancars AMEN.
Bw. Joachim Mushi ambaye ni Mhariri wa makala wa Gazeti la Jambo Leo akiuaga mwili wa marehemu mke wake Primtiva Pancras kwa majonzi makubwa wakati wa ibada ya kuaga mwili huo iliyofanyika kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mpiga picha wa New Habari Cooparation 2006 Anthony Siame pamoja na muombolezaji mwingine wakimsaidia mmoja wa waombolezaji aliyeshindwa kujizuia mara baada ya kuona mwili wa marehemu Primtiva Pancras na kupoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni leo.
Mdau Jerry Muro mbele kulia na mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima Absalom Kibanda nyuma pamoja na waombolezaji wengine wakiwa aktika ibada hiyo ya mazishi leo.
Rais amteua Balozi Malambugi kuwa Balozi Mpya nchini Brazil!!
Posted by
ADMIN
Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Balozi Francis Malambugi kuwa Balozi wa Tanzania Brasilia nchini Brazil .
Uteuzi wa Balozi Malambugi umefuatia kutokana na aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Balozi Daktari Joram Mkama Biswaro kuteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika.
Balozi Malambugi ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria na Mwanadiplomasia alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 1/1/1978 kama Wakili wa Serikali na amewahi kufanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Angola, Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Geneva, Ujerumani,Ethiopia na Ubelgiji.
Jaji Eliamani Mbise afariki dunia
Posted by
ADMIN
Kumradhi wasomaji wetu tumeondoa picha tuliyoichapisha katika habari hii kwa kuwa tuliiweka kimakosa kwani picha hiyo siyo ya marehemu Eliamani Mbise tunaomba radhi kwa usubufu wote alioupata mhusika katika picha hiyo lengo letu lilikuwa ni zuri katika kupasha habari makosa ya kiutendaji yalifanyika.
Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Eliamani Mbise amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa. Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Msajili wa Mahakama ya Rufani Francis Mutungi imesema Jaji Mbise imesema Jaji Mbise amefariki majira ya saa nne na nusu tarehe 29/7/2010 .
Taarifa hiyo imesemakuwa taratibu za mipango ya Mazishi ambayo yatafanyika Arusha itatolewa baadae baada ya utawala kuwasiliana na ndugu wa marehemu.
Aidha Bwana Mutungi amesema msiba umewekwa kwa muda nyumbani alipokuwa akiishi marehemu Mikocheni kwenye nyumba za viongozi wa Serikali.
Marehemu Mbise alikuwa akifanya kazi katika kituo cha kazi cha Mahakama kuu ya Tanzania .
WAFANYAKAZI WIZARA YA HABARI WAKUTANA.
Posted by
ADMIN
Subscribe to:
Posts (Atom)