Umoja wa mataifa umeonya kuwa ghasia za kikabila zinazoendelea nchini Kyrgyzstan, huenda zikasambaa hadi nchi jirani ikiwa hazitakomeshwa mara moja.
Kwa mujibu wa msemaji wa umoja huo, Rupert Colville jamii za watu wa Tajikistan na Uzbekistan pamoja na jamii zingine za makabila madogo Kyrgyzstan , wanakabiliwa na tisho kwa usalama wao.
Inakisiwa watu 170 wameuawa kwenye ghasia hizo za siku nne.
Umoja wa mataifa umesema utachunguza ripoti kuwa mauaji na ubakaji nchini Kyrgyzistan yamepangwa kwa misingi ya kikabila.
Umoja wa mataifa umesema utachunguza ripoti kuwa mauaji na ubakaji nchini Kyrgyzistan yamepangwa kwa misingi ya kikabila.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Kyrgyzstan, Almazbek Otumbayev, amedai ghasia hizo zilikuwa zimepangwa na wafuasi wa rais aliyeondolewa Kurmanbek Bakiyev, madai ambayo ameyakanusha.
Urusi imesema haitatuma vikosi vya kuweka amani kwa sasa. Afisa wa serikali ya Urusi ameiambia BBC kwamba mkutano wa dharura uliofanyika mjini Moscow ulikubaliana kutuma misaada ya chakula na mablanketi.
Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi limetangaza mipango ya dharura ya kupeleka misaada kwa ndege nchini Uzbekistan kwa wakimbizi 75,000 wa asili ya Uzbek waliokimbia kutoka Kyrgyzstan
0 comments:
Post a Comment