WAREMBO MISS ILALA WATEMBELEA OFISI ZA VODACOM TANZANIA!!

Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akiwakaribisha warembo katika kitengo cha masoko cha kampuni hiyo wakati warembo hao wanaoshiriki shindano la Miss Ilala walipotembelea katika makao makuu ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania jengo la PPF Tower jijini Dar es salaam jana jioni, leo ndiyo warembo hao watapanda jukwaani kuchuana wakiwania taji la Miss Ilala 2010 kwenye shindano litakalofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza katika picha wa nne ni mtaalam wa habari Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.
Sylivia Shally Miss Ilala 2009 akiongea jambo wakati wa hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya warembo hao wanaoshiriki shindano la Miss Ilala leo katikati ni Rukia Mtingwa Meneja Matukio na Mdau mwingine kutoak Vodacom Tanzania.
Warembo wa Redds Miss Ilala wakifanya onesho dogo wakati walipotembelea ofisi za Vodacom Tanzania jana jioni.
Mrembo akitembea kwa madaha kuonyesha jinsi watakavyotembea leo katika shindano lao linalofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
Warembo wakijimwaga kucheza muziki wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili yao wakati walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania jengo la PPF Tower jana jioni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment