Meneja mkuu wa global publishers akikabidhi msaada kwa wagonjwa katika wodi ya watoto kwenye Hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Sekondari Jangwani, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wodi wa Watoto na Global Publishers baada ya kukabidhiwa misaada yao.
Global Publishers, wachapishaji wa magazeti pendwa nchini, leo Alhamiswametembelea wodi ya watoto wadogo wenye matatizo ya kuvimba vichwa(Hydrocephalus), na kutoa misaada ya kibianadamu kama vile sabuni,mafuta ya kujipaka, pampers, Dettol, nk. Wodi hiyo iko ndani yaHospitali ya Taifa ya Muhimbili na ina takriban watoto 30 wenyematatizo hayo, na wengi wao wanatoka nje ya Dar es salaam.Jambo la kusikitisha kuhusu watoto hawa, wengi wao baada ya kuzaliwawamesuswa na akina baba hivyo mzigo wote kuachiwa akina mama.
Kutokanana kutokuwa na ndugu katika jiji la Dar es salaam, akina mama haohukosa mahitaji muhimu hata ya sabuni kwa ajili ya kufua nguo zawatoto wao ambao hujisaidia haja ndogo na kubwa kila wakati wakiwakitandani.Ingawa serikali inatoa huduma ya chakula na matibabu kwa watoto haobure na chakula kwa wazazi wao, ambao hulazimika nao kukaa wodini nawatoto wao, lakini wanahitaji misaada ya kibanadamu kwa wingi, kwanihali ni mbaya, na wakati mwinginehukosa hata kipande cha sababu chakufua mikojo ya watoto wao. Wito unataolewa kwa wadau wenginekuwakumbuka akina mama hawa.
Aiddha, Global Publishers imetoa misaada ya chakula na bidhaa zingineza usafi kwa wanafunzi walemavu wa shule ya Sekondari ya Jangwanijijini Dar es salaam, ambao nao hupata huduma mbalimbali za matibabukatika Hospitali hiyo ya Taifa.Wanafunzi hao, ambao wako kidato cha kwanza hadi cha nne, wote niwalemavu na wanatembelea viti vya magurudumu. Nao wanahitaji sanamisaada ya kibinadamu.
0 comments:
Post a Comment