TFF BADO MLIKUWA NA NAFASI YA KUPATA BILIONI TATU



Timu za TANZANIA na BRAZIL ziliimeingiza shilingi bilioni moja nukta saba katika mchezo wa kirafiki uliofanyika June 7 mwaka huu katika uwanjawaTAIFA JijiniDSM
Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini FREDRICK MWAKALEBELA amesema haijawahi kutokea kupata mapato kama hayo katika mechi zote zilizowahi kufanyika katika uwanja huo.
Amesema ni rekodi nzuri kuona kuwa watanzania wanajitokeza kuishangilia timu yao ya TAIFA pindi inapokuwa inacheza.
Katika hatua nyingie katibu MWAKALEBELA amesema katika mchezo huo wa kiarafiki kati ya TANZANIA na BRAZIL wachezaji sita wa TAIFA STARS wamependwa na baadhi ya mawakala nchini kutokana na kiwango chao kizuri.
Hivyo TFF inamatumaini na wachezaji hao huenda wakapata nafasi ya kwenda kucheza soka nche ya nchi.
Hata hivyo bado nawashauri TFF kuwa kiwango hicho hakiridhishi kutokana na mchezo wenyewe hasa kutokana na timu yetu kucheza na timu ya Brazili ambayo ni timu maarufu duniani kwani kama kiingilio cha walala hoi ambao ndiyo wapenda soka sana kingefikiriwa na kuwepo, ni dhahiri kwamba uwanja wa taifa ungefurika mashabiki wengi na hilo pengo la hasara ya Bilioni moja nukta tatu lingeweza kuzibika kama si kupata faida zaidi katika mchezo huo.
Mimi kwa uelewa wangu mdogo katika soka siamini kwamba wale mashabiki waliojitokeza katika uwanja wa Taifa ndiyo ulikuwa mwisho kwa maana kwamba hakukuwa na mashabiki wengine waliotaka kwenda kuangalia mchezo huo na sijawahi kuona Brazili wanacheza huku uwanja ukiwa na mapengo yaani haujajaa, mara nyingi huwa naona uwanja umejaa katika michezo ya kirafiki wanayochezwa na timu hiyo katika nchi tofautitofauti .
Naamini kama TFF ingepunguza angalau kiwango fulani kwa viti vya kijani na Bluu mashabiki wengi wangeweza kujitokeza kuangalia mchezo huo, hivyo ni vyema mkaliangalia hili katika wakati ujao ili kila mpenda soka hata wa hali ya chini aweze kupata nafasi ya kuona na ninyi mweze kuongeza zidi mapato kwa viingilio

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment