Muigizaji maarufu wa filamu nchini Steven Kanumba leo alifumwa na Camera ya FULLSHANGWE kiwa katika kaofisi kake kapya huko Ilala Boma akionekana yuko bize kwa kung'arisha viatu vya wateja wake, ambapo amekuwa akipata wateja wengi sana kiasi kwamba wapita njia hujaa na kuangalia ni kitu gani anafanya mwigizaji huyo.
Habari hii ilinifanya na mimi nivutiwe na kujua kile kilichomvutia mwigizaji huyo mpaka akaamua kwenda kuanzaisha kaofisi hako kapya ambako inaelekea kanamwingizia ngawila za kutosha kwa siku.
Hata hivyo Steven Kanumba alionekana kucheka wakati alipokuwa akinipa maelezo yake ambapo alisema hiyo ni moja ya Location ya filam u yake mpya inayokwenda kwa jina la
(More Than Pain) hebu tusubiri ili tuone itakuwaje wadau kaeni mkao wa kula.
0 comments:
Post a Comment