BENKI ya KCB Tanzania imezindua promosheni ya kuuza baadhi ya hisa zake chini ya bei ya awali lengo likiwa ni kukuza kiwango cha mtaji wa kampuni hiyo kubwa kanda ya Afrika Mashariki ikiwa rasilimali ni dola za Kimarekani 2.6.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uuzaji huo wa hisa mshauri wa masuala ya kibiashara wa benki hiyo Amish Gupta alisema kwamba mpango huo mahususi umekuja ili pia uwawezeshe wanahisa wa KCB kununua hisa nyingi za benki hiyo.
Akifafanua Gupta alisema kuwa kwa sasa wateja, wadau na wanahisa wa benki hiyo watanunua hisa moja ya KCB Tanzania kwa bei 310/- kutoka 385/- bei iliyokuwa ikitumika katika kipindi cha wastani wa miezi sita iliyopita punguzo likiwa ni sawa na asilimia 21.
“Mpango huu unaotarajiwa kuanza rasmi Julai moja utakamilika Julai 23 mwaka huu na kwamba wanahisa waliofanikiwa kununua hisa za benki yetu kupitia kwa mwaka huu,” alisema Gupta.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa wakala wetu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa punguzo la bei watatajwa Agosti 5 alisema hisa zitakazonunuliwa zitatumika katika nchi zote ambako benki hiyo inatoa huduma na zinauzwa kwa wananchi wote hata waso wateja wa benki hiyo.
Alisema pesa zitakazokusanywa zitatumika kupanua wigo wa utoaji huduma nchini na sio kwenye matawi ya nje ili kuongeza kiwango cha utoaji mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na uendelezaji wa makazi.
0 comments:
Post a Comment