HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA ILIANDIKWA JANA BARANI AFRIKA!!

Rais Jacob Zuma akizindua mashindano hayo jana kwenye uwanja wa Soccer City jana wakati timu yake ya Bafanabafana ilipowakaribisha Mexico kwenye mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya kombe la Dunia nchini Afrika Kusini jana Multchoice walikuwa na sherehe kubwa waliyoiandaa kwenye klabu ya Savanah Lounge Paradise Hotel jijini Dar es salaam ambapo waliwakaribisha wadau mbalimbali ili kushuhudia mchezo hu wa ufunguzi huku wakipata kinywaji na kuangalia sherehe hizo za ufunguzi kupitia luniga kubwa mbili zilizokuwa zimefungwa ukumbini hapo ilikuwa ni bradani tosha kwani kwa mara ya kwanza historia mpya ya kombe la dunia iliandikwa likichezwa kwa mara ya kwanza katika ardhi ya bara la Afrika toka lianzishwe.

wadau Agness na Dina nao hawakukosa mtanange huo.

Mdau Ronald Shelukindo kulia, Barbara Kambongi nwa mdau mwenzao kutoka Multchoice Tanzania.

Hawa ni Wadau Kapya wa Ecco Bank, Robert, Abdulmajid Nsekela na Maurice Njowoka wa NMB Bank.

Shabiki huyu wa Afrika kusini akishangilia kwa nguvu hebu mcheki mdau.

Wadau kutoka Busness Time wakishangilia mara baada ya afrika kusini kupata goli jana.

Mzee Salim Try Again akifuatilia kwa karibu mpambano huo kwenye klabu ya Savanah Laonge.

Wadau waliojitokea ili kushuhudia mpambano huo kati ya Afrika Kusini na Mexico jana ambapo timu hizo zilitoka szre ya magoli 1-1. kutoka kulia ni Jef,Durell, Albert na Kay.

Hapa akiikagua timu yake ya Afrika Kusini.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Sepp Blatter Rais wa Shirikisho la mpira duniani FIFA wakiwa uanjani tayari kwa kweeka Historia ya bara la Afrika.

Timu ya Taifa ya Afrika Kusini Bafanabafana ikliwa uwanjani.

Dr. Khumalo mchezaji wa zamani wa timu ya Bafanabafana na mwenzake John Barns mchezaji wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza wakiwa studio za Supersport Afrika Kusini jana katika kuchambua mpira huo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Nd. Bukuku, picha ya chini kabisa, kulia, ni John Barnes mchezaji wa zamani wa |Liverpool na England ambaye katika world cup hii yuko South Afrika akiwa mmoja wa wana jopo wa Supersports.

Post a Comment