Mgeni rasmi Naibu waziri wa Wizara ya Miundombinu Mh. Ezekiel Chibulunje katikati akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya makampuni ya ujenzi yalioandaliwa na Bodi ya ya usajili wa Makandarasi CRB ambapo wadau mabalimbali wa mambo ya ujenzi, Mitambo na vifaa mbalimbali vya ujenzi vinaonyeshwa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, maonyesho hayo ni ya siku mbili yaliambatana na mkutano mkuu wa mashuriano kati ya Bodi ya usajili na makandarasi yanafanyika leo na kesho.
Waliopo katika picha kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya usajiri CRB Charles Kitwanga, Msajili wa bodi ya Makandarasi Boniface Muhegi na kutoka kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu Miundombinu Eng. Omary Chambo na mwisho kushoto ni Jovita kutoka CRB.
Mkurugenzi wa maosoko wa Shirika la Bima la Tanzania Aloyce Mwasuka kushoto akimuelezea jambo mgeni rasmi Naibu Waziri wa Miundombinu Mh. Ezekiel Chibulunje alipotembelea banda hilo mara baada ya kuzindua rasmi maonyesho hayo yaliyoandaliwa na bodi ya Makandarasi nchini CRB.
Wadau kutoka CBA wakiwa katika banda lao kutoka kushoto ni Theresia Soka, David Shambwa, Aron Luhanga na Kunegunda Dedede benki ya CBA ni wadhamini wa maonyesho hayo yaliyoanza leo na yatamalizika kesho jioni.
Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la bima la Taifa NIC Tanzania Ltd Aloyce Mwasuka katikati akiwa na maofisa kutoka shirika hilo katika banda lao kwenye maonyesho ya bodoi ya makandarasi CRB yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee, kulia ni Juma Kiungulia na kushoto ni Paschal Kimolo.
0 comments:
Post a Comment