CHAMA CHA MCHEZO WA KUOGELEA CHAWAFUNDA MAKOCHA WAKE!!

Kocha wa taifa wa mchezo wa kuogelea John Belela akitoa semina kwa makocha wa mchezo hu kutoka mikoa mbalimbali nchini iliyoandaliwa na chama hicho kwa lengo la kuwaweka makocha hao katika madaraja mbalimbali, semina hiyo imefanyika kwenye uwanja wa uhuru leo.
Katika Semina hiyo mada zilizojadiliwa ni (Phisology) jinsi gani mwili wa mchezaji unafanya kazi (Safety) jinsi ya kuwa salama wakati wa mazoezi na mashindano(Differentition) jinsi ya utofautishaji wakati wa mazoezi na wakati wa mashindano juu ya kujali jinsia uhuru na mazingira(Ethics) Maadili ya Makocha pamoja na Wachezaji na (Promotion) Jinsi ya kuukuza mchezo wa kuogelea.
Watoa mada walikuwa ni Alexander Mwaipasi Rais wa chama cha KuogeleaRamadhani Namkoveka Kocha Amina Mfaume John Belela Kocha wa Taifa na Lameck Borega.
Makocha kutoka mikoa mbalimbali wakifuatilia kwa karibu maelezo ya kocha wa taifa wa mchezo wa kuogelea John Belela hayupo pichani.

Kutoka kulia ni Alexander Mwaipasi rais wa chama cha kuogelea nchini, Amina Mfaume katibu wa chama na Michael Livingstone Mkurugenzi wa Habari

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment