NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
21/05/2020
NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Joel Bendera amewataka Watanzania kuzingatia na kuenzi tamaduni zao ili kuimarisha amani nchini hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Bendera katika kilele cha maadhimisho ya Utamaduni Duniani Kanda ya Mashariki yaliyofanyika kwenye uwanja wa sabasaba jijini Dar es Salaam, ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Utamaduni ni Kichocheo cha Amani”.
“Nina imani kuwa endapo kila mmoja wetu atauenzi utamaduni wake,hakutakuwepo na mamabo maovu kama ya utoaji na upokeaji rushwa, ugomvi unyanyasaji wa kijinsia, ujambazi ,uporaji mauaji ya kinyama yanayofanywa na aina fulani ya watu, kwani hakuna tamaduni zozote za Kitanzania zinazoruhusu mambo hayo,” alisema Waziri Bendera.
Alisema amani inapatikana kwa njia nyingi, shibe inaleta amani,Ndiyo maana taifa letu limeamua kuanzisha sera ya ya kilimo kwanza ili kuhakikisha kwamba nchi inapata chakula cha kutosha na cha ziada.
Waziri Bendera alisema kuwa changamoto inayowakabili Watanzania ni kutekeleza sera hiyo ili kuepuka kuwa tegemezi huku akiwataka Watanzania kufanya kazi halali kwa bidii na kuepuka vijiwe.
Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri yatakayoweza kuimarisha biashara za utamaduni.

0 comments:
Post a Comment